Habari za Punde

*BAADA YA KUTIMULIWA NCHINI KENYA MWANAMUZIKI KOFFI OLOMIDE SASA KUSHITAKIWA NCHINI CONGO

BAADA ya wiki iliyopita kutimuliwa nchini Kenya Mwanamuziki nguli wa muziki wa Dansi nvhini Congo, Koffi Charls Antwaa Olomide, sasa kubebewa bango na Shirika la kutetea haki za binadamu la Asvoko, lililoiomba Serikali ya nchi hiyo kumfungulia mashitaka mwanamuziki huyo na kumburuza Mahakamani. 

Shirika hilo limeiomba Serikali kumshitaki mwanamuziki huyo baada ya Ijumaa ya Wiki iliyopita kuonekana katika video iliyosambaa mitandaoni akimpiga teke mmoja wanamuziki wake wa kike kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi jambo lililomsababisha kutimuliwa nchini humo.

Baada ya tukio hilo na sakata la kutimuliwa nchini Kenya, nalo Shirika la Zambia la Kilimo na Biashara limeamua kufuta Tamasha la Mwanamuziki huyo lililokuwa limepangwa kufanyika nchini humo kati ya Jumatano hadi Jumatatu Ijayo. 
Akizungumzia taarifa hiyo, Raisi wa Taasisi hiyo Ben Shoko, alisema kitendo hicho alichokifanya mwanamuziki huyo wa kimataifa wa muziki wa dansi sio cha kiungwana kabisa, 
Na ndiyo sababu iliyopelekea wao kulifuta Tamasha hilo.
Ijumaa iliyopita katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata JKIA Nairobi Koffi alinaswa katika video akimpiga teke dansa wake huyo kwa kilichodaiwa alikorofishana na mwanamuziki wa kundi hilo aitwaye Cindy Le Couer ambaye amekuwa na mahusiano naye ya kimapenzi toka 2012.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.