Na Zainab Ally Hamis, Dar es salaam School of Journalism (DSJ)
Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band a.k.a FFU yenye makao yake Makuu nchini Ujerumani, wanatarajia kupanda jukwaani kupiga bonge la shoo katika maonesho ya Afrika-Karibik, siku ya jumamosi Julai 16 Julai 2016 mjini Bayreuth, Ujerumani.
Katika Tamasha hilo kubwa la 'International Afrika Festival Tubingen',
Julai 30, 2016 watatumbuiza XXL Afro Summer Jam mjini Stuttgart katika Kutur Arena. mzimu huo wa muziki wa bongo dansi utaendelea kudatisha mashabiki Agosti 13, 2016 mjini Frankfurt katika Afro-Karibik viwanja vya Robestock Park, Frankfurt,Ujerumani.
Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya imefanikiwa kujiongezea maelfu ya mashabiki kwa wingi.
Bendi hiyo inayoongozwa na mwanamuziki nguli Ebrahim Makunja. a.k.a kamanda Ras Makunja wa FFU, itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika maonyesho hayo makubwa na ya aina yake kwa mashabiki wa muziki katika maonyesho hayo, ambapo watakumbana "Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band.
Bendi hiyo kwa sasa inatamba na nyimbo zake za, Mapenzi ya Pesa, na single CD ya, La Mgambo, Supu ya Mawe, Uhuru wa Habari, na Bongo Tambarare, ambazo zipo katika CD ya BONGO TAMBARARE zote zinasikika katika kambi ya FFU au web yao ya www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com




No comments:
Post a Comment