Habari za Punde

*JULIO ATAMBA KUONYESHA MAAJABU NA KUCHUKUA UBINGWA MSIMU UJAO

Na Zainab Nyamka, Dar
KOCHA mkuu wa Mwadui FC ya Mkoani Moshi, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa msimu huu wamejipanga kuanza na kasi mpya na ya aina yake baada ya kuamua kufanya marekebisho kwenye kikosi chao na kupunguza idadi ya wachezaji.
''Kwa maandalizi tunayoyafanya kipindi hiki na sisi tutakuwa kama Leiciester City wa Tanzania na tumejipanga kufanya maajabu makubwa msimu ujao'', alisema Julio
Awali Mwadui ilikuwa na wachezaji takribani 33 na sasa wameamua kupunguza idadi hiyo na kufikia wachezaji 24.
Aidha Julio amesema, kwa msimu huu wamejipanga zaidi kuwezw kufanya vizuri na zaidi wameshazoea mikikimikiki ya Ligi. Katika msimu uliopita hawakuweza kufanya vizuri kutokana na ugeni wao kwenye mashindano hayo na kuwataka makocha wa timu nyingine kukaa chonjo na kujiandaa kikamilifu na wasitegemee mtelemko.
"Timu yangu msimu huu itakua ni zaidi ya moto wa kuotea mbali kwani msimu uliopita hatukufanya vizuri kutokana na ugeni wetu ila kwa sasa wajipange sana na sisi ndio tutakuwa Leiciester ya Tanzania yoyote akija mbele yetu ataambulia kipigo tu ,"amesema Julio.
Kocha huyo mwenye kariba ya kuchonga sana, amesema kuwa mshambuliaji Paul Nonga aliyerejea kwenye kikoso hicho hana tatizo nae kwani wakati anaondoka aliondoka kwa adabu na kuwaaga na kupewa baraka zote na Klabu hiyo.
''Nonga alikuwa anatafuta maisha na hata baada ya kushindwa na kuamua kurudi nyumbani tumempokea kwa mikono miwili'' alisema Julio
Nonga msimu wa 2015/16 mzunguko wa pili alijiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini ameshindwa kupata namba ya uhakika.kwenye kikosi cha mholanzi Hans Van De Pluijm na kuishia kukaa benchi na wakati mwingine kutokupangwa kabisa na kuamua kuachana na wanajangwani hao na kurudi Mwadui Fc.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.