Mtendaji
Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja akicheza mpira wa meza
na Mkufunzi wa Shirikisho la Dunia kutoka Egypty Ahmed Dawlatly baada ya
ufunguzi wa mafunzo hayo katika Shule ya Msingi Kisutu leo asubuhi
Mtendaji Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja akizungumza na waandishi wa habari na kutoa maelekezo kwa Viongozi wa TTTA (hawapo pichani) kuhusu kupanua wigo wa mchezo huo katika vituo vingine Mkoa wa Dar es salaam pamoja na mikoa mingine. Kushoto ni Mkufunzi wa Mpira wa Meza wa Shirikisho la mchezo huo la duninia kutoka Egypty Ahmed Dawlatly.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja hayupo pichani wakati akifungua mafunzo.
Mtendaji Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkufunzi wa Mpira wa Meza wa Shirikisho la mchezo huo la dunia kutoka Egypty Ahmed Dawlatly (kushoto), Kaimu Mwenyekiti wa TTTA Athony Mutafurwa (kulia) baada ya ufunguzi.
**************************************
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo
la Taifa (BMT) Bw. Mohamed Kiganja ameitaka Kamati ya Oliympiki Tanzania (TOC)
wajiulize na kujifunza jinsi nchi zingine zinavyokuza na kuendeleza michezo kupitia
kamati hizo.
Rai hiyo ameitoa leo wakati akifungua
mafunzo ya Ualimu wa Mpira wa Meza yanayofanyika kwa siku nane kuanzia tarehe 4
hadi 11 Julai mwaka huu katika Shule ya Msingi Kisutu jijini Dar es salaam.
Aidha, ameitaka Kamati hiyo kuweka wazi
kwa vyama mambo wanayotakiwa kuyafanya kuendeleza michezo wanayoelekezwa na
Kamati ya Olimpiki ya dunia.
“TOC jengeni mahusiano yakaribu na muwe
wawazi kwa vyama, mpo kwa ajili ya kuendeleza michezo, fanyeni vile mnavyoelekezwa
na Kamati hii duniani”, alisema Kiganja.
Katika hatua nyingine Kaimu Katibu Mkuu
wa Baraza Bw. Mohamed Kiganja amekielekeza chama cha mchezo wa meza kupanua
wigo kwa kuanzisha vituo vingine katika
Manispaa za Kinondoni na Temeke na katika shule tofauti za Mkoa wa Dar es
salaam na wasitegemee kituo kimoja cha shule ya Kisutu pekee.
Aliendelea kuwa, chama hakina budi
kwenda mbali zaidi katika Mikoa mingine ambapo, aliwahakikishia kuwa, Baraza liko tayari kuwasaidia kwa Makatibu
Tawala ili kuona mchezo huo unakuwa katika Mikoa yote nchini.
“Tuwatengenezee mazingira Walimu
wanaopata mafunzo”, alieleza.
Awali Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Meza
(TTTA) Bw. Athony Mutafurwa ameeleza changamoto zinazokikabili chama cha mpira
wa meza ni pamoja na Uwanja na fedha ambapo ameeleza kuwa, TTTA inaishauri
Serikali kurudisha mfumo wa kutoa ruzuku kwa vyama na kuongeza kuwa:
Serikali ione umuhimu wa kujenga uwanja
wa ndani wenye hadhi ya kimataifa katika awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa
Taifa ili Tanzania tuweze kuandaa mashindano ya kimataifa ambayo yamekewa
yakishindikana kutokana na kukosekana kwa uwanja.
No comments:
Post a Comment