Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akisikiliza maelezo kutoka kwa
mwenyekiti wa serikali za mtaa wa (TPDC)Bw,
Idrisa Hashimu kuhusu Uchafuzi wa Mazingira Unaofanywa na viwanda katika mtaa
huo.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa katika ukaguzi wa Mazingira katika kiwanda cha MMI steel kinachotuhumiwa Kuchafua mazingira katika mtaa wa TPDC.
*****************************************
Na Evelyn Mkokoi, Dar
Kiwanda cha kutengeneza vyuma cha MMI
Steel kilichopo katika eneo la viwanda mikocheni jijini Dar es Salaam, kimetozwa
faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa kulipa faini hiyo baada ya siku saba
kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka 2004, kwa kutiririsha
maji machafu katika maeneo ya mtaa wa TPDC kwa warioba jijini dar es salaa.
Maji ambayo ni hatari kwa mazingira na viumbe hai.
Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea
eneo la mtaa wa viwanda mikocheni
kufuatia uchafuzi wa mazingira unaotokanao na utitiririshaji wa majitaka katika
maeneo hayo.
Wakati huohuo, Shirika la maji safi
na majita taka Jijini Dar es Salaam na Pwani
( Dawasco) limepewa siku kumi na saba kumaliza tatizo la utiririshaji wa
maji taka katika mtaa wa TPDC mikocheni kwa Warioba jijini Dar es Salaam.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu
Waziri Mpina Baada ya kufanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi wa tatu na
kutoa siku saba kwa DAWASCO na NEMC kusimamia suala zima la usafi wa mazingira
na agizo lake kuupuzwa.
Awali, Mhe. Mpina alisema kuwa
uchafuzi wa mazingira hauwezi kuendelea kuvumiliwa na lazima hatua za kisheria
zichukuliwe, na kuwaasa watendaji wa taasisi za serikali kuyapa kipaumbele
maagizo yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu za serikali kinyume na hapo ni
kutokutii mamlaka. “tasisi za serikali lazima zifanye kazi kwa kushirikiana
kutokana na kwamba kumekuwa na kutupiana mpira kati ya NEMC, dawasco na
Manispaa ya kinondoni katika suala zima la utatuzi wa uchafuzi wa mazingira
katika mtaa wa TPDC.” Alisema.
Naibu waziri Mpina aliongeza kuwa ifikapo tarehe 30/7/2016 asikutane tena na tatizo la uchafu na harufu
mbaya katika mtaa wa TPDC kwani hali hiyo ni hatari sana kwa afya ya wakazi wa
maeneo hayo na mazingira.
Kwa upande wake DAWASCO ikiwakilishwa
na Injinia Erick Jackson alisema kuwa Tangu muheshimiwa Naibu Waziri Mpina atoe
agizo la uondoshwaji wa majitaka na uboreshwaji wa miundombinu katika mtaa huo,
wamekuwa wakifanya kazi na bado inaendelea na kazi hiyo pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali
za kifedha na ufundi.
Hata hivyo uongozi wa Halmashauri ya
wilaya ya kinondoni umelishitaki shirika la maji safi na maji taka jijini dar
es salaam na Pwani DAWASCO ,kiwanda cha MMI steel na Tembo Tiles kwa uchafusi
wa mazingira kwa kutirirsha maji taka.
No comments:
Post a Comment