Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto akikabidhiwa madawati na Bi Malidadi kwa niaba ya mkurugenzi wa Kilolo ,madawati hayo yametengenezwa kwa mfuko wa jimbo la Kilolo yaliyogharimu kiasi cha Tsh milioni 30 awali madawati hayo yalikataliwa kutokana na kutengenezwa chini ya kiwango.
Dc Kilolo Asia Abdalah na timu ya wataalam wakijiridhisha na ubora wa madawati hayo ambayo sasa yapo safi
Mbunge Mwamoto akifurahia ubora wa madawati ya mfuko wa jimbo la Kilolo
**************************************************
Na Mwandishi Wetu, Iringa
MADAWATI 745 ambayo yalitengenezwa na mfuko wa jimbo la Kilolo kwa gharama ya Tsh milioni 30 zilizotolewa na mbunge wa jimbo hilo Venance Mwamoto ambayo yalikataliwa na mbunge huyo na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza yamekamilika kutengenezwa kwa ubora .
Akizungumza baada ya kukabidhiwa madawati hayo leo mbunge Mwamoto alisema kuwa amekubali kupokea madawati hayo baada ya kufurahishwa na ubora wake na hivyo imani yake kuona walimu wanasimamia utunzaji wa madawati hayo ili kuondokana na kero tena ya madawati katika shule zote za wilaya ya Kilolo.
Mbunge Mwamoto alisema kuwa kufuatia uhaba wa madawati uliokuwa ukiikumba wilaya ya Kilolo na kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilazimika kuidhinisha pesa kiasi cha Tsh milioni 30 kutoka mfuko wa jimbo la Kilolo ili kuweza kusaidia utengenezaji wa madawati 300 japo Halmashauri ya Kilolo kupitia wadau wake wa ndani na makusanyo ya ndani waliweza kuongeza kiasi cha Tsh milioni 19 na kufanya kuwepo kwa kiasi cha pesa cha Tsh milioni 49 ambazo zilifanikisha kutengeneza madawati zaidi ya 1000 .
"Nililazimika kukataa madawati 40 ambayo yalipelekwa shule ya Msingi Nyanzwa na Igunda baada ya kuyaona hayana ubora na wananchi kulalamika kuwa ni mabovu ukilinganisha na madawati ambayo yalitengenezwa kwa nguvu ya wananchi katika vijiji hivyo ......hivyo sikuwa tayari kupokea madawati hayo hali iliyopelekea mkuu wa mkoa wa Iringa kufika kuona madawati hayo na kulazimika kuyakataa madawati yote 745 kwa kutaka yatengenezwe kwa ubora"
No comments:
Post a Comment