Habari za Punde

*POLISI KIGOMA WAUA MAJAMBAZI WAWILI BAADA YA MAJIBIZANO YA RISASI

 ACP OBADIA NSELU akionyesha magazini iliyokamatwa katika tukio hilo
***********************************
Na Abel Daud, Kigoma
Majambazi wawili ambao hawakuweza kufahamika majina yao,wamefariki dunia wakiwa njiani kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu, kutokana na kuvuja damu nyingi, baada ya kujeruhiwa kutokana na majibizano ya kutupiana risasi na Askari Polisi.
Akizungumza naWaandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP.OBADIA NSELU, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Julai 19- katika barabara kuu ya Wilaya ya Buhigwe-bukuba, katika eneo la msitu wa koli kata ya buhigwe tarafa ya manyovu Mkoani Kigoma.
Aidha kamanda NSELU ameongeza kuwa kupitia majibizano ya risasi dhidi ya Askari polisi na majambazi hao, majambazi walizidiwa nguvu ndipo idadi ya majambazi isiyojulikana walitokomea na kuingia msituni.
Baada ya Askari polisi kuwadhibiti majambazi hao waliweza kukamata siraha moja aina ya SMG yenye namba za usajili 13303136 ikiwa na magazini moja na risasi 16.
Katika tukio jingine, Kamanda NSELU ameongeza kuwa kupitia operation zinazo fanywa na kikosi cha usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali zisababishazo vifo na majeruhi kwa wananchi,kwa mwaka 2015 kuanzia januari hadi disemba jumla ya watu 82 Mkoani Kigoma walifariki dunia kutokana na ajari za barabarani huku jumla watu 122 wakijeruhiwa katika ajari hizo.
Ameongeza kuwa kwa kipindi cha mwaka 2016 kuanzia januari hadi june jumla ya watu 44 wamepoteza maisha yao kutokana na ajari za barabarani huku jumla ya watu 53 wakiwa wamejeruhiwa.
 Kaimu kamanda wa Mkoa wa Kigoma ACP OBADIA NSELU akijibu moja ya swali aliloulizwa na mmoja wa waandishi wa habari.
 ACP OBADIA NSELU akionyesha magazini iliyokamatwa katika tukio hilo
Pikipiki zilizokamatwa katka oparetion inayoendelea ya kudhibiti ajali zinazopelekea vifo na majeruhi

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.