Habari za Punde

*TETESI, KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA MSERBIA DRAGAN POPADIC KUTUA AFRICAN LYON

TETESI zilizoeneo hivi sasa katika Soka la Kibongo ni kuhusu aliyewahi kuwa Kocha wa zamani aliyeipa mafanikio makubwa Klabu ya Simba Mserbia, Dragan Popadic, aliyetua nchini kukinoa kikosi cha African Lyon iliyorejea Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu wa 2016/17.
Pamoja na kuenea kwa tetesi hizo lakini bado Uongozi wa Klabu hiyo haujaweka wazi juu ya ujio wa Kocha Popadic, kuhusu kukinoa kikosi hicho msimu ujao.
Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu Mmiliki wa African Lyon, Rahim Kangezi Zamunda,alisema kuwa mpaka sasa bado haijathibitishwa rasmi kuhusu Kocha atakayekinoa Kikosi hicho.
Na alipoulizwa kuhusu ujiowa Kocha wa zamani wa Simba, Mserbia Dragan Popadic, Zamunda alisema kuwa Kocha huyo amekuja kutembea na kufanya shughuli zake na kuamua kuwatembelea katika mazoezi yao na kuendelea kukanusha habari zinazozidi kuenea kwamba bado hawajaamua na kumtangaza kocha atakayekinoa kikosi cha African Lyon.
Pamoja na kukanusha huko lakini, habari za chini ya Kapeti zinasema kuwa Kocha huyo aliyekuwa akiifundisha Klabu ya Coffee ya Ethiopia, bado anaendelea na mazungumzo na Uongozi wa African Lyon ili kufikia muafaka wa kubaki nao msimu uajo.
Lyon imerejea tena kwenye ligi baada ya kushuka na kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu uliopita ambapo inaungana na timu ya Ruvu Shooting na Mbao FC zilizopanda kucheza ligi kuu msimu ujao.

MAFANIKIO YA POPADIC AKIWA NA KIKOSI CHA SIMBA MIAKA YA NYUMA
Popadic aliiwezesha Simba kutwaa mataji kadhaa ambapo kati ya mwaka 1994 na 1996 alibeba mataji saba, mawili ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ambayo kwa sasa ni Kagame, 1995 na 1996, ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo, 1994 na 1995, ubingwa wa Ligi ya Muungano mwaka 1994 na ubingwa wa Kombe la Nyerere miaka ya 1994 na 1995.
Popadic aliichukua timu hiyo kutoka mikononi mwa kocha Abdallah Kibadeni aliyesaidiana na Mhabeshi, Etienne Eshente waliokuwa wametoka kuifikisha Simba katika Fainali za Kombe la CAF mwaka 1993 ambapo Wekundu wa Msimbazi walipoteza fainali hiyo kwa mabao 2-0 dhidi ya Stella Abdijan.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.