Kivuko cha Magogoni katika hatua za kukamilishwa ukarabati wake. Kivuko hiki kinatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni, Mkoani Dar es Salaam
Sehemu ya juu ya Mlango wa kivuko cha Magogoni. Wa pili kulia ni Mhandisi Lekujan Manase (Mtendaji Mkuu TEMESA) akimuelekeza jambo Major Songoro (Mkurugenzi kutoka kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd inayokarabati kivuko hicho) mwenye shati la “blue” Picha zote na Theresia Mwami,TEMESA
Kivuko kipya cha Mv Pangani katika hatua za kukamilishwa kwa ujenzi wake, unaofanyika katika eneo la bandari ya Dar es salaam.
Wakikagua mtambo wa kuendeshea kivuko (propulsion unit), kutoka Kushoto ni Mhandisi Lekujan Manase (Mtendaji Mkuu TEMESA), Major Songoro ( Mkurugenzi kutoka Songoro Marine Transport Ltd), Vitus Bujimu (Mwakilishi Kutoka Songoro Marine Transport Ltd), Mhandisi Lazaro Vazuri ( Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme), Mhandisi Japhet Maselle ( Mkurugenzi wa Huduma za Vivuko kutoka, TEMESA) pamoja na Mhandisi Dkt. William Nshama (Mkurugenzi,Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme)
No comments:
Post a Comment