Na Daudi Manongi, MAELEZO
Wakala
wa Vipimo Tanzania imewafungulia kesi mahakamani wafanyabiashara saba waliokuwa wakifanya
uchakachuaji wa mizani za kupimia Pamba ambapo kati ya kesi hizo nne zimetolewa
hukumu na wafanyabiashara hao wamelipa faini na zilizobakia ziko mahakamani.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Meneja
wa Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala
wa Vipimo (WMA), Irene John alipokuwa akieleza hatua
zilizochukuliwa hadi sasa baada ya
kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wakulima wa pamba hususani kanda ya
ziwa.
Bi.Irene amesema kuwa kila ukifika msimu wa pamba wanunuzi
hao hutumia mizani iliyochakachuliwa na kuwaibia wakulima na hivyo msimu huu
ulivyoanza wakatuma maofisa wao katika vituo vyote vinavyonunua pamba ili
kuhakikisha uuzaji wa pamba unafanyika kwa kutumia vipimo sahihi kwa lengo la
kumlinda mkulima na katika ukaguzi huo wamefanikiwa kukamata wafanyabiashara
hao wasio waaminifu.
Aidha amesema kuwa kabla ya kutuma wataalamu wake,
wakala wa vipimo(WMA) ilituma wataalaumu wake kuzunguka mikoa yote inayolima pamba hususani Kanda ya Ziwa ili kutoa elimu kwa wakulima na
wafanyabiashara kuacha udanganyifu huo kwani unaathiri sekta nzima ya kilimo
hicho.
Aliongeza kuwa uchakachuaji huu umeifanya pamba ya
Tanzania kila inapofika katika soko la dunia kushushwa bei kwa kukosa ubora
ukilinganisha na zamani ambapo pamba ya
Tanzania iliitwa dhahabu nyeupe kwenye soko la dunia na kuchukua alama ya
kwanza kwa ubora wa pamba yetu, hivi sasa hali imebadilika baada ya kuzuka
mchezo huo michafu.
Kaimu Meneja uyo wa Elimu,Habari na Mawasiliano
amewaasa pia wakulima kuacha mtindo wa kuweka maji, mchanga na hata mawe ili
kupata kilo nyingi katika pamba kwani vinaathiri mbegu na hivyo kupotea thamani
ya zao lenyewe na kuhaidi zoezi hili la ukaguzi litaendelea mpaka msimu wa pamba
utakapoisha mwezi wa nane.
Aidha amesema kuanzia mwaka huu adhabu ya
uchakachuaji wa mzani wa kupimia pamba ni faini ya shilingi elfu 50 au miaka
mitatu jela.

No comments:
Post a Comment