KOCHA Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaanzisha pamoja Mzimbabwe, Donald Ngoma, Mrundi Amissi Tambwe na Mzambia Obrey Chirwa katika safu ya ushambuliaji katika mchezo dhidi ya Medeama FC, leo.
Yanga inawakaribisha Medeama FC ya Ghana jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika.
Na Pluijm amerudia karibu kikosi chake kile kile kilochompa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, langoni akimuweka Deogratius Munishi ‘Dida’, mabeki; kulia Juma Abdul, kushoto, Oscar Joshua na katikati Kelvin Yondani na Vincent Bossou.
Viungo ni Mbuyu Twite na Thabani Kamusoko katikati, wakati pembeni ni Simon Msuva na Chirwa, washambuliaji ni Tambwe na Ngoma.
Wachezaji wa akiba ni Ally Mustafa ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Makapu, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi, Malimi Busungu na Andrew Vincent
KIKOSI CHA MEDEAMA:
Daniel Adjei, Samuel Adade, Moses Sapong, Paul Adu, Daniel Amouah, Kwesi Donsu, Erick Kwakwa, Kwame Boahene, Abbas Mohamed, Bernard Ofori na Enock Atta.

No comments:
Post a Comment