Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera
na Uratibu), Dk.Hamis Mwinyimvua (kulia) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika
uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha
waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao.Kulia kwake ni Katibu
Mtendaji Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Bengi Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari na kuwahimiza watanzania kushiriki kikamilifu katika kongamano la siku mbili la ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha waanchi wake wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
*******************************************************
Na Daudi Manongi, MAELEZO Dar es Salaaam
SERIKALI
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa kongamano kongamano la siku mbili la
uwekezaji litakalojadili mipango madhubuti ya kuhakikisha Watanzania
wanashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.
Kongamano
hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Dar es Salaam
kuanzia tarehe 21 -22 Julai mwaka huu.
Hayo
yamesemwa leo Jijiji Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na
Uratibu) Dkt.Hamis Issa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu
kongamano hilo.
Dkt.
Issa alisema Serikali imepitisha Sera ya ushiriki wa watanzania katika sekta ya
Mafuta na Gesi asilia, hatua ambayo itasadia wananchi wazawa kushiriki
kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa nchi yao.
“Msukumo mkubwa wa serikali kwa sasa ni kuongeza
ushiriki katika uwekezaji unaochochewa
na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kina kirefu cha bahari ambao utaweza kuwanufasha Watanzania” alisema Dkt. Issa.
Aidha
alisema kuwa kutokana ushiriki huo wa Watanzania kuwa suala mtambuka na agenda
endelevu, Serikali iliiagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji kuanzisha Idara ya
ushiriki wa watanzania katika uwekezaji ambayo imeanza kutekeleza majukumu yake
mwezi Novemba mwaka 2015.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Beng’i Issa alisema
kuwa katika kongamano hilo linatarajia kushirikisha jumla ya wajumbe 350 wakiwemo
wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, Watendaji wa Serikali Kuu na
halmashauri za Miji na Majiji.
Akizungumzia
kuhusu manufaa ya kongamano hilo, Beng’i
alisema Watanzania watanufaika zaidi kwa kuwa wataongeza ujuzi na uzoefu katika
kushirikiana na wafanyabiashara wakubwa waliopo nje ya nchi wanaojihusisha na sekta
za mafuta, gesi, kilimo, fedha, bima, ujenzi na manunuzi ya umma.


No comments:
Post a Comment