Habari za Punde

*WAZIRI WA MWAKYEMBE AONGEA NA AFISA MIPANGO WA MASUALA YA USAJILI NA VIFO WA TAASISI YA BLOOMBERG YA MAREKANI

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo wakati wa kikao na Afisa Mipango wa Masuala ya Usajili wa Vizazi na Vifo wa Taasisi ya Bloomberg ya Marekani Bw. James Mwanza (wa kwanza kulia kwa Waziri). Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watendaji wakuu wa RITA, kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar Es Salaam.
Afisa Mipango wa Masuala ya Usajili wa Vizazi na Vifo wa Taasisi ya Bloomberg ya Marekani Bw. James Mwanza (wa pili kushoto) akiongea kuhusu masuala mbalimbali ya Usajili wa Vizazi na Vifo katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome 
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watendaji wakuu wa RITA, wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) na Afisa Mipango wa Masuala ya Usajili wa Vizazi na Vifo wa Taasisi ya Bloomberg ya Marekani Bw. James Mwanza (wa kwanza kulia kwa Waziri) baada ya kikao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.