Waombolezaji wakilishusha jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Marehemu Joseph Senga, wakati wa maziko yake yaliyofanyika wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza leo Agosti 1, 2016. Marehemu Senga alifariki wiki iliyopita nchini India alikokuwa akipatuiwa matibabu ya moyo. Mungu ailaze roho ya marehemu Senga mahala pema peponi AMIN.
Wawakilishi wa Chama Cha Wapiga Picha Tanzania, Said Powa, (kushoto), na Emmanuel Herman, wakiwa kwenye ibada yamaziko.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na mmiliki wa Gazeti la Tanzania Daima, alilokuwa akifanyia kazi marehemu, akitia mchanga kaburini.
Mbunge wa Nsuve Richard Ndasa, ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu akimuaga kwa mara ya mwisho kabla ya maziko yake leo.
Mama wa marehemu akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na ndugu.
Mama wa marehemu akimuaga mwanae huku akisaidiwa kugusa mwili wa mwanae kwa mara ya mwisho kabla ya maziko.

Mke wa marehemu, Bi Winfrida Senga akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mumewe.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mpigapicha Mkuu wa gazeti hili, marehemu Joseph Senga wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika Kijiji cha Shushi Wilaya ya Kwimba, Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndassa akiweka shada la Maua.
Ibada ya Mazishi ikiendelea.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiweka shada la maua kaburini.













No comments:
Post a Comment