Habari za Punde

*MOURINHO AANZA NA VITIMBI MAN U, AMUINGIZA MATTA NA KUMTOA

Lilikuwa ni jambo la kushangaza kwa watu wengi waliolitazama pambano la kungombea ngao ya Hisani ikimaanisha ufunguzi wa Ligi kuu ya Uingereza kati ya mabingwa wa ligi hiyo Leicester City na mabingwa wa FA Manchester United, pale kocha wa Man U Jose Mourinho, alipomuingiza kipindi cha pili Juan Matta kuchukua nafasi ya 
mfungaji wa bao la kwanza la United Jesse Lingard, ambaye alipata maumivu ya mguu 
na kumtoa nje dakika chache baadaye, katika 
dakika ya 63. 

Jose Mourinho lisema kuwa alichukuwa uamuzi wa kumtoa Mata ili kuweza kuzuia mipira ya juu iliyokuwa ikielekezwa langoni mwa timu yake, ‘ilinilazimu kumuingiza mtu mwenye kimo kirefu kidogo ili aweze kucheza mipira mirefu ya juu isilete madhara langoni mwetu” alisema Mourinho. 

Mata mwenye umri wa miaka 28 ambaye inasemekana angeondoka Manchester United katika siku za hivi karibuni alionekana kuchanganyikiwa alipotolewa nje katika dakika za mwisho za mchezo ambapo Manchester United waliweza kupata ushindi na kubeba ngao hiyo ndani ya dimba la Wembley. 

Mourinho ambaye alimuuza Mata kutoka Chelsea kwenda Man United msimu wa 2013-14 anasema alifanya mabadiliko hayo kwa lengo la kuiokoa timu yake isipoteze mchezo huo. “Alicheza vizuri na alinipa kile nilichotaka” Mourinho alliiambia BT Sport. “Kanuni zinaruhusu kufanya mabadiliko ya wachezaji 6,mimi nilitaka kumaliza mchezo nikiwa nimebakiwa na mtu mmoja tu wa kumbadilisha,ilibidi niangalie yupi ni mdogo (mfupi) nisinge mtoa Zlatan au Fellain kwani wapinzani wanacheza mipira ya juu hivyo mtu pekee alikuwa Mata”. Aliongeza “najua alikasirika lakini alielewa kwani kila mmoja alitaka ushindi hivyo wote tumefurahi”. 

Ibrahimovic ameweka alama ndani ya United baada ya kufunga bao la ushindi dakika saba kabla ya mchezo kumalizika,ikiwa nikufuatia bao lakuongoza la United lililofungwa na Lingard na lile la kusawazisha la Leicester lililofungwa na Jame Vardy.
 Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, akitoa maelekezo kwa mchezaji aliyeingia kuchukua nafasi ya Juoan Matta.
 Mshambuliaji mpya wa Man U, Ibrahimovic, akishangilia bao lake aliloifungia timu yake katika mchezo wa jana dhidi yao na Leicester City. Katika mchezo huo
 Jose Mourinho (kushoto) akisalimiana na Kocha wa Leicester City, baada ya mchezo huo kumalizika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.