Makabidhiano ya funguo yakiendelea baina ya Meneja wa Wakala wa majengo Mkoa wa Mwanza Eng. Yohana Mashausi na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo nchini ndugu Francis Assenga, huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mwenye kofia akishuhudia tukio hilo
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo kwa Wakulima nchini akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella mapema kabla ya makabidhiano hayo kwenye eneo la tukio
Jengo hapa likifunguliwa tayari kukaguliwa na kukabidhiwa kwa wahusika.

***************************************************
Na. Atley Kuni- Mwanza
Wakulima wa
mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla wameshukiwa na neema ya pekee
kufuatia jitihada za serikali ya awamu
tano kuwaanzishia Benki yao katika kanda hii, ambayo itakuwa na makao
yake makuu katika Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa
mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza wakati wa makabidhiano wa jengo
litakalo tumika kwa ajili yashughuli za kibenki kwa kanda ya ziwa lakini pia
kama tawi kwa mkoani wa Mwanza, amesema Sekta ya kilimo ambayo hubeba zaidi ya
asilimia 80 ya wananchi wa Tanzania kwa sasa imepatiwa mkombozi.
“Kama
mnavyo fahamu, sekta hii ina mnyororo mrefu, wapo wanao lima, wengine
wanachakata mazao lakini wapo pia wanao safirisha mazao kwendanje ya nchi na
wengine wanao leta mzao ndani ya nchi, alisema Mongella na kuongeza,
“tunavyozungumzia asilimia 80% ni hawa wote, tunataka mwisho wa siku kilimo
kimlipe mtu na kuendesha maisha yake” alisema Mkuu wa Mkoa.
Kwa upande
wake, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Kilimo Nchini, Francis Assenga,
yeye amesema shabaha yakufunguliwa kwa benki hiyo nikutaka kumkomboa mkulima
kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuingia katika kilimo cha kibiashara,
“Tukasema tuangalie sehemu ambayo inamatokeo ya haraka lakini eneo ambalo
linachangia kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa, tukasema Mwanza ni mahali
sahihi”. Alisema Assenga.
Amesema
kanda ya ziwa inayo miradi mingi ya kilimo hasa wingi wa viwanda ambavyo vitatumika, katika kusindika
, kuchakata na kufanya kilimo cha biashara ambapo mnyororo wa thamani ulivyo
kwa kanda ya Mwanza.
Mkurugenzi
huyo, amesifu pia utayari wa Viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa
Mkoa kwa utayari walio uonesha lakini pia kutafuta eneo ambalo Benki hiyo
itakuwepo, “Kimsingi tumefurahishwa sana na utayari wa Mkuu wetu wa Mkoa John
Mongella, akisema anatenda, sasa miongoni mwa kanda sita tunazo kwenda
kuzianzisha Mwanza inakuwa kanda ya kwanza kwani fedha tayari zimetolewa na
serikali kwa ajili ya uanzishwaji wa Benki hii” alisema Assenga.
Katikati ya
Makabidhiano hayo, Mha ndisi wa Majengo katika Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Yohana
Mashausi, akasema wao wapo tayari kwaajili yakuwakabidhi Benki ya wakulima
Jengo ambalo lilikuwa likitumiwa na Mamlaka ya mapato (TRA) hapo kabla.
No comments:
Post a Comment