Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa uamuzi wa kutengua uteuzi
wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na uteuzi wa
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola.
PIX2: Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akifafanua jambo mbele yanwaandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola na kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano wao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) alipokuwa akitangaza uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na wajumbe saba wa Bodi ya baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija - MAELEZO
*******************************************************************
Frank
Mvungi –Maelezo
Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba (Mb)
ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Usimamizi
wa Mazingira (NEMC) na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ili kuongeza tija na
kutekeleza kwa vitendo dhana ya Ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo Waziri chini ya Sheria ya Mazingira
kifungu cha 19 (2) anaweza kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Baraza hilo na
wajumbe wake.
Akizungumza
na vyombo vya Habari leo Jijini Dar es Salaam Waziri Makamba amesema kuwa lengo
la mabadiliko hayo ni kuhakikisha kuwa kunakuwa na usimamizi na uzingatiaji wa
Sheria ya Mazingira na uharakishaji wa
miradi ya maendeleo na uwekezaji hasa ujenzi wa viwanda kama azma ya Mheshimiwa
Rais John Magufuli inavyoelekeza.
Kufuatia
mabadiliko hayo Waziri Makamba amemteua Dkt. Elikana Kalumanga ambaye ni
Mhadhiri katika Taasisi ya Usimamizi na Tathmini ya Rasilimali Asili,Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NEMC hadi Rais atakapoteua Mkurugenzi
Mkuu.
“Utendaji
wa NEMC umekuwa ukilegalega sana na umekuwa hauridhishi na kumekuwepo na
malalamiko mengi kutoka kwa wawekezaji
wa ndani na nje ya nchi kuhusu ucheleweshaji na urasimu usiokuwa wa
lazima katika mchakato wa tathmini ya athari kwa mazingira (EIA)” Alisisitiza
Mhe. Makamba
Aliongeza
kuwa ametengua uteuzi wa wajumbe wote saba wa Bodi ya NEMC ili baadaye ateue
wajumbe wapya ambao wataendana na kasi na ari ya Serikali ya Awamu ya Tano
katika kuelekea uchumi wa Viwanda, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ambaye mamlaka
yake ya uteuzi ni Mheshimiwa Rais,ataendelea kuwepo hadi Mheshimiwa Rais
atakapoteua mwingine.
Akifafanua
Makamba amesema kuwa changamoto nyingine zilizobainika ni kuwaelekeza
wawekezaji kwa makampuni ya kufanya Tathmini ya athari za mazingira ambayo
yanamilikiwa au yenye ubia na watumishi wa NEMC, bila kujali mgongano wa
kimaslahi jambo ambalo haliruhusiwi katika utumishi wa umma.
Jambo
jingine ni kuwarundikia maandiko ya miradi ya tathmini ya athari kwa mazingira
(EIA) watumishi wachache wakati wengine hawana kazi ili waelekeze miradi hiyo
katika makampuni ambayo baadaye huwapatia malipo yasiyo halali.
Hatua
nyingine zilizochukuliwa na Waziri Makamba ni pamoja na kuiagiza NEMC kufuta
watu binfsi na Makampuni yote ya ushauri wa EIA (Consultants) ambayo hayana
sifa au yameshindwa kutekeleza kazi zao vizuri na watangaze kwenye magazeti orodha ya watu na makampuni yanayoruhusiwa
kufanya kazi kama washauri elekezi.
Baraza
la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC ni muhimu katika kuhakikisha
ustawi wa mazingira na mustakabili wa maendeleo endelevu ya nchi tunapoelekea
kuwa Taifa la uchumi wa viwanda lazima usimamizi wa mazingira uwe thabiti.
No comments:
Post a Comment