Katibu mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(katikati)
akieleza jambo wakati wa kuwakaribisha wataalamu 16 kutoka nchni Cuba wakiwemo Madaktari Bingwa 6
pamoja na Wauguzi wa Chumba cha
uangalizi maalumu kwa wagonjwa mahutiti mapema leo Hospitali ya Taifa
Muhimbili Jijini Dar es Salaam kushoto ni kiongizi mkuu wa matibabu nchini
Tanzania Dkt. Maylen Lopezi na kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya
taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Cuba katika hafla ya kuwakaribisha katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jijini Dar es Salaam.
Na Agness Moshi
na Pascal Dotto-MAELEZO.
Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea wataalamu 16 kutoka nchini Cuba kama moja
ya mikakati yake ya kuboresha utoaji huduma za Afya ikiwemo kutoa huduma za
kibingwa hapa nchini.
Akiongea
na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dk.Mpoki Ulisubisya alisema kuwa
Serikali imepokea madaktari bingwa 6, madaktari bingwa wa usingizi 2, madaktari
wa wodi za wagonjwa mahututi 2, Daktari bingwa wa upasuaji wa macho 1, mtaalamu mmoja wa
radiolojia pamoja na wauguzi 10 wa vyumba vya wagonjwa mahututi.
“Wataalam
hawa mamekuja wakati muafaka, kwasababu kwa kipindi hiki hospitali ya Muhimbili
inafanya maboresho ya utoaji huduma , hivyo nina amini uwepo wao hapa kwa miaka
miwili, hautakuwa kwa ajili ya kuboresha
huduma au kusaidia wagonjwa tu , bali ni nafasi nzuri ya kuwapa ujuzi na mafunzo wataalamu wetu “,alisema Dk.Ulisubisya.
Dk. Ulisubisya amesema kuwa uwepo wa wataalamu hao utaongeza nguvu kazi
hususani kwenye utoaji huduma kwa wagonjwa mahututi kwani hospitali hiyo
imeongeza vitanda vya wagonjwa mahututi kutoka vitanda 21 hadi 88.
Dk.
Ulisubisya ameongeza kuwa wataalamu hao watasaidia kupunguza msongamano kwenye
wodi za wagonjwa mahututi pia kupunguza idadi ya wagonjwa kwenda nje kwa ajili
ya matibabu kwani huduma za matibabu zitapatikana hapa nchini.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Prof.Lawrence Museru amesema kuwa,
kutokana na uhaba wa wataalamu kwa kipindi hiki cha maboresho,Hospitali
imetafuta wataalamu kutoka Cuba ili kuziba pengo hilo.
Prof.Museru
alisema kuwa kwa kipindi chote cha miaka miwili,wataalamu hao watatoa mafunzo
kwa wataalamu wa hapa nchini ambao utawapa ujuzi na kuwasaidia katika maeneo ya
utoaji huduma kama vile huduma za upasuaji macho,wagonjwa mahututi ,radiolojia
,na usingizi.
Aidha,Dkt.Ulisubisya
ametoa wito kwa Taasisi nyingine za Afya nchini,kuiga mfumo unaofanywa na
hospitali ya taifa Muhimbili ili kusaidia kupunguza utegemezi serikalini katika
kuboresha huduma za Afya.
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeweka mikakati
mbalimbali ya kuboresha utoaji huduma
ikiwa ni pamoja na kuongeza wodi za wagonjwa mahututi,Ununuzi wa vifaa tiba,kukarabati
na kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 13 hadi kufikia 20, pamoja na
kukabiliana na changamoto ya rasilimali watu kwa kupelekeka wataalamu nje ya
nchi kwa ajili ya mafunzo.
No comments:
Post a Comment