Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) akisalimiana na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph Nyamhanga (Kushoto) wakati
alipokaribishwa katika ofisi za Wizara leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni
Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na Wa pili kushoto Katibu
Mkuu Dkt. Maria Sasabo (Sekta ya Mawasiliano).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Kushoto), akisalimiana na Naibu Waziri Eng. Atashasta Nditiye (Kulia), wakati alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akizungumza na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam,
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), mara baada ya kuapishwa Jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia), leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu wa wizara na baadhi ya Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akiwakabidhi manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa wakati (Katikati) vitabu vya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 ya Wizara hiyo kama mwongozo wa utendaji kazi mara baada ya kuapishwa jijini Dar es Salaam leo.
*****************************************
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote katika
sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na
ushirikiano katika kuwahudumia Watanzania ili kufikia malengo ya Wizara.
Prof. Mbarawa ameyasema
hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano ofisini Jijini Dar Es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Dar es Salaam
“Mimi nafurahi sana
kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu mimi
na wafanyakazi tuko katika timu moja; tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano.
Katika kipindi cha miaka miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbali mbali ya
serikali mfano ujenzi wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.
Akiwakaribisha Manaibu Mawaziri hao katika
Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi
kupata mawaziri wapya ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
“Sisi kama viongozi tunapaswa kuwa mfano
katika utendaji wetu wa kazi ili kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu.
Tunapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio
masuala ya msingi katika utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema
Waziri amesema Wizara
hiyo imefanya kazi nzuri na hili limewezekana kwa sababu sisi kama wizara
tumezingatia maadili ya msingi katika utendaji wa kazi zetu, kuna timu nzuri ya
watalaam ambao ni wachapa kazi, wana moyo wa kujituma na kazi zote
walizozifanya zina matokeo mazuri.
Kazi nzuri imefanyika,
nawaomba waheshimiwa manaibu mawaziri
tufanye kazi kama timu moja na watalaam wetu ili tuweze kufikia malengo ambayo
tumejiwekea katika wizara yetu, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Kwa upande wake Naibu
Waziri anayeshughulikia Eng. Atashasta Nditiye anayeshughulikia Sekta ya
Uchukuzi na Mawasiliano amesema kuwa amejipanga kufanya kazi na kulete matokea
chanya na kwa maendeleo ya nchi.
“Nipo tayari kufanya
kazi itakayoleta mabadiliko, tutaboresha miundombinu ili kuchochea kasi ya
ukuaji wa viwanda na kila nitakachofanya ni utekelezaji wa yale amabayo Mhe.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli anayatarajia,” amesema mhandisi Nditiye.
Hii ni mara ya kwanza
kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri tangu serikali yake iingie madarakani
Novemba 2015.
No comments:
Post a Comment