Baadhi ya vitanda vilivyohamishwa wagonjwa katika
wodi mbalimbali kwenye jingo la Mwaisela Hospitalini Muhimbili kwenda Hospitali
ya Tiba na Taaluma Mloganzila kufuatia utekelezaji wa agizo la Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto la kuhamisha wagojwa katika
jingo hilo hivi karibuni.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea baadhi ya wodi zilizohamishwa wagonjwa kwenye jingo la Mwaisela kufuatia agizo alilolitoa la kuhamisha wagonjwa kwenye jingo hilo kuhamia Mloganzila wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa muhimbili kuangalia utekelezaji wa agizo lake.
Waziri wa Afya,maendewleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kulia akimjulia hali mtoto Maria (17) mkazi wa Mtwara aliyetangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ana uvimbe mkubwa wakati alipokwenda kumtembelea kwenye Taasisi ya Mifupa MOI jijini Dar es salaam. PICHA NA WIZARA YA AFYA.
*************************************************
*************************************************
NA
WAMJW-DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameridhishwa na utekelezaji wa agizo la kuhamisha
wagonjwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kwenda Hospitali ya Tiba na
Taaluma Mloganzila.
Hayo ameyasema wakati alipotembelea Hospitali ya
Taifa Muhimbili ili kuangalia hali ya utoaji wa huduma pamoja na utekelezaji wa
agizo hilo alilolitoa wakati alipotembelea Hospitali ya Tiba na taaluma
Mloganzila mapema mwezi huu.
“Niliwaagiza MNH kuhamisha wagonjwa waliopo kwenye
jingo la Mwaisela kuaznia wodi namaba 3,4,5,6,7 na 8 isipokuwa wagonjwa
mahututi na wenye kesi maalumu ila nawapongeza wametekeleza agizo hilo mara
moja” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amewapongeza MNH kwa kuwahamisha madaktari bingwa 15 15 na wauguzi zaidi ya 30 kwenda katika
Hospitali ya Mloganzila ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma sawa na inayotolewa
Muhimbili.
Mbali na hilo Waziri Ummy amesema kuwa zoezi hilo limetoa
nafasi ya kuwahamisha baadhi ya wagonjwa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) hususani watoto angalau vitanda 50 kupeleka kwenye jingo la Mwaisela
hospitali ya MNH.
“JKCI ni moja wapo ya Taasisi zinazotoa matibabu ya
upasuaji hasa ya moyo na ina upungufu wa majengo hivyo kutokana na uhamishwaji wa wagonjwa
jengo la Mwaisela tunawapa nafasi ya kupeleka vitanda 50 kwa ajili ya wagonjwa
wao waliofanyiwa upasuaji hususan watoto” aliongeza Waziri ummy.
Sambamba na hilo Waziri Ummy alipata muda wa kwenda
kumtembelea Mgonjwa alikuwa analalamika kwenye baadhi ya vyombo vya habari
ajulikanaye kwa jina la Maria (17) mkazi wa Masasi Mkoani Lindi kuwa ana uvimbe
mkubwa na akalizimika kuletwa katika Hospitali ya Taifa yMuhimbili.
“ Niliposikia habari ya Binti huyo kwenye baadhi ya
vyombo vya habari niliomba namba za wahusika na kuwaelekeza waende Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili na hivi sasa anapata matibabu kwenye taasisi ya Mifupa (MOI)
na wanaendelea na juhudi za kumtibia ili kumrudsha katika hali yake ya zamani”
alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alitoa rai kwa Watanzania kuwa
wanatakiwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa madaktari bingwa na kuacha imani
potofu kwa kwenda kwa waganga wa kishirikina kwa kuamini mgonjwa atakuwa
amerogwa ili kuepuka tatizo kuwa kubwa zaidi.
“Kwa mujibu wa madaktari wamesema kuwa Maria
alihudhuria hospitali hapo mara mbili na hakurudi tena kama ilitakiwa afanye na
badala yake akajikita zaidi kwenye tiba asili mpaka imesababisha tatizo kuwa
kubwa zaidi hivyo watanzania tunatakiwa kuwaamini zaidi madaktari na kufuata
maelekezo” alisema Waziri Ummy.




No comments:
Post a Comment