Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, enzi za uhai wake.
**********************
Habari zilizotukia asubuhi hii zinasema kuwa Mwanasiasa Mkongwe nchini, Kingune Ngombale-Mwiru, amefariki Dunia alfajiri ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa kipindi cha mwezi mmoja akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam.
Mwanzoni mwa mwezi Januari, Mkewe, Peras Ngombalemwiru, pia alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kupooza wakati Mzee Kingune akiwa amelazwa akipatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kung'atwa na mbwa. MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU KINGUNE MAHALA PEMA PEPONI, AMEEN


No comments:
Post a Comment