Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege Mwanza, Bi. Easter Madale (kushoto), alipokagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho mkoani Mwanza leo.
Meneja wa Kiwanja cha Ndege Mwanza, Bi. Easter Madale (wa pili kushoto), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), eneo ambalo litajengwa uzio wa kiwanja hicho, mara baada ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho mkoani Mwanza leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu mipango ya Serikali ya kuendeleza kiwanja cha Ndege Mwanza kwa kuiboresha miundombinu ili kiwanja hicho kiwe cha Kimataifa, wakati alipokagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushotoa), akikagua maendeleo ya ujenzi barabara ya Pasiansi hadi Airport KM 4.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza.
Muonekano wa sehemu ya barababara ya Pasiansi hadi Airport KM 4.6, inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza.
Muonekano wa jengo
la kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwanza, ambapo ujenzi wake umekamilika
kwa asilimia 80, na linajengwa na kampuni ya Beijing Construction Engineering
Group (BCEG).
*******************************************
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa
Mamlaka ya Viwanja Ndege Nchini (TAA), kukusanya fedha za madeni ambayo inadai kutoka
kwa watoa huduma mbalimbali katika viwanja vyote vya ndege ili ziweze kutumika
kuendeleza miundombinu.
Kauli
hiyo ametoa jijini Mwanza, baada kukagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja cha
ndege na hali ya uendeshaji katika kiwanja hicho ambapo amebaini kuwa kuna
madeni ambayo yanaweza kulipika na kuweza kurahisisha shughuli za kiuendeshaji
ikiwemo kujenga uzio ili kuongeza usalama kiwanjani hapo.
"Nataka
TAA mkusanye madeni yote mnayodai, fedha hizi zikipatikana zinaweza kutumika
kujenga uzio kwa ajili ya kulinda usalama wa uwanja ili wananchi wasiweze
kuvamia na pia usalama wa ndege zinazoruka na kutua", amesisitiza Prof.
Mbarawa.
Amefafanua
kuwa kama Taasisi hizi zikikusanya madeni na watoa huduma wakalipa kodi kwa
wakati kutasaida Serikali kuboresha maendeleo ya miundombinu.
Kuhusu
maendeleo ya upanuzi wa kiwanja hicho. Prof. Mbarawa amesema ameridhishwa na
kasi ya ujenzi ambapo kwa sasa umefikia asilimia 60.
Ameongeza
kuwa ujenzi huo unategemewa kumalizika mwezi Julai mwaka huu na utagharimu
kiasi cha shilingi takribani bilioni 94.
Aidha
amesema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la
abiria mara miradi inayoendelea kukamilika.
Naye
Msimamizi wa Kiwanja hicho ambaye ni Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS),
mkoa wa Mwanza, Mhandisi Joseph Mwami, amesema
kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa jengo la kuongoza ndege,
eneo la maegesho na njia za kuruka na kutua ndege
Mhandisi
Mwami, amefafanua kuwa njia ya kuruka na kutua ndege katika kiwanja hicho
imeongezwa urefu wa mita 500 ili kuifanya kufikia urefu wa KM 3.5 ili kuwezesha
ndege kubwa za kimataifa kuweza kutua na kuruka katika kiwanja hicho.
Katika
hatua nyingine Waziri Prof Mbarawa amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa
barabara ya Mwaloni-Pasiansi-Airport yenye urefu wa KM 5.3 kwa kiwango cha lami
ambapo ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika
mwezi mei mwaka huu na utagharimu kiasi cha shillingi bilioni 9.5.
"Nimekagua
na niwapongeze Kampuni ya wazawa ya Nyanza Road kwa kazi nzuri mliyofanya
katika ujenzi kwa barabara hii", amesema Prof Mbarawa.
Waziri
Prof. Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kutunza na kulinda miundombinu hiyo kwa
manufaa ya kuongeza tija na maendeleo kwao kwan inapunguza msongamano wa magari
kwa kiasi kikubwa na Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kugharamia
utekelezaji wa miradi hiyo.
Waziri
Prof Mbarawa yuko mkoani mwanza kwa ziara ya siku akiwa na lengo la kukagua
utekelezaji wa miundombinu ya sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment