Na Amina Kasheba, Dar
SHIRIKISHO la filamu Tanzania (TAFF) linatarajia kuandaa mafunzo ya uandishi wa script ya filamu.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Mathew Bicco, amesema kwa sasa wanajiandaa na mafunzo hayo ambayo yatakuwa na tija kwa waandishi wa filamu zetu.
Aidha Bicco aliongezea kuwa kwa sasa Shirikisho lipo katika mchakato wa kuandaa mashindano ya undishi wa filamu, kati ya mwezi Aprili na Mei mwaka huu ambapo washiriki watakuwa ni waigizaji pamoja na watayarishaji.
''Mashindano hayo tunatarajia kuanza baada ya kumalizika kwamafunzo hayo ambapo tunatarajia kupata waandishi bora wa filamu kutoka mikoa tofauti.
Katika shindano hilo tutaangalia vipengele mbalimbali katika sekta ya filamu”, amesema.
Taff kwasasa inakabiliana na wauzaji feki wa kazi za filamu ambazo inasababisha kushuka kwa soko la filmu nchini na kufanya wasanii kushindwa kunufaika na kazi zao.

No comments:
Post a Comment