Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani) kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (Hawapo Pichani)kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo, Bw. Richard Mkumbo Picha-Wizara ya Fedha na Mipango
*******************************************************
Ndugu
Wawakilishi wa vyombo vya habari, nimewaiteni leo hii ili
niwape taarifa fupi kuhusu malipo ya madai ya malimbikizo ya mishahara kwa
Watumimishi wa umma waliokuwa na madai ili muweze kuufikishia umma wa
Watanzania.
Serikali kupitia mfumo wa
taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System
– HCMIS) kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya
mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111
Wakiwemo walimu 53,925 waliokuwa wanadai shilingi 53,940,514,677.23 sawa na asilimia 42.27 ya madai yote, na wasiokuwa walimu 28,186 waliokuwa wanadai
jumla ya shilingi 73,664,614,195.58 sawa na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai
haya yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017
Madai haya yalijumuisha
mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za
mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa
mishahara.
MATOKEO
YA UHAKIKI WA MADAI YA SHILINGI BILIONI 127,605,128,872.81 KWA WATUMISHI 82,111
a)
Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi 43,393,976,807.23
ikiwa ni asilimia 34 ya madai
yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81 yaliyohakikiwa
yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.
b)
Madai yanayostahili kulipwa
yanajumuisha shilingi bilioni 16.25
kwa walimu 15,919 na shilingi bilioni
27.15 kwa watumishi wasiokuwa
walimu 11,470
c)
Madai yote yaliyoonekana kuwa sahihi ya shilingi bilioni 43.39 yatalipwa pamoja na
mshahara wa mwezi Februari 2018 kwa mkupuo mmoja. Malipo ya Madai haya ambayo
mengine yana zaidi ya miaka kumi majina ya walipwaji wote yatatangazwa kwenye
magazeti kuanzia kesho tarehe 10 Februari, 2018.
Kwa matokeo hayo
ya uhakiki, mazoezi yaliyofanyika likiwemo
zoezi la kuwaondoa kwenye Mfumo wa malipo ya mshahara (“payroll”)
watumishi hewa, vyeti feki na wasio kuwa na sifa na uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara
uliofanyika limeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 84.22 ambazo ni sawa na asilimia 66 ya madai yote ya malimbikizo ya
awali ya shilingi bilioni 127.61 yaliyokuwa
kwenye mfumo ambazo bila zoezi la uhakiki
kufanyika zingelipwa wakati zilikuwa hazistahili kulipwa.
Serikali
itaendelea kulipa madai ya watumishi kadiri yanavyojitokeza ili kuondokana na
malimbikizo ya aina hii ambayo yanaweza kuisababishia Serikali hasara kwa
kulipa madai yasiyostahili.
Asanteni
kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment