TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MATOKEO YA OPERESHENI
MAALUM ILIYOFANYIKA MJINI MAGHARIBI- ZANZIBAR, KUANZIA TAREHE 14 – 21.03.2018
Ndugu Wanahabari,
1.
UTANGULIZI ;
Zipo taarifa kuwa baadhi ya wananchi Mkoa
wa Mjini Magharibi wanatumia, wanashiriki, wanafadhili au kusaidia biashara ya
madawa ya kulevya kama ilivyo kwenye maeneo mengine nchini.
Hata hivyo Serikali ipo kwenye vita kali ya kupambana na mtandao wa madawa
ya kulevya na Inspekta Jenerali wa Polisi kwa kushirikiana na Kamisheni ya Polisi
Zanzibar waliunda timu kutoka Kitengo cha Operesheni Maalum za Polisi Makao
Makuu Dar es salaam kuja kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa kero hii kama ilivyo
kwenye maeneo mengine ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2.
MATOKEO YA OPERESHENI ;
|
S/N
|
MAFANIKIO
|
MATOKEO / IDADI
|
|
TAARIFA ZA
INTELIJENSIA
|
||
|
1.
|
Kupatikana
kwa taarifa za watuhumiwa
wanaojihusisha na mtandao wa madawa ya kulevya (kutumia, kuuza, kufadhili au
kusaidia)
|
105
|
|
JUMLA KUU
|
105
|
|
|
WATUHUMIWA WALIOPATIKA NA HATUA
|
||
|
1.
|
Watuhumiwa
waliofikishwa Mahakamani
|
26
|
|
2.
|
Watuhumiwa
waliopo chini ya Upelelezi
|
16
|
|
3.
|
Watuhumiwa
waliopo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee)
|
16
|
|
JUMLA KUU
|
58
|
|
|
VIELELEZO
|
||
|
1.
|
Heroin
|
Kete 1293 na Vifuko 3 sawa na
Gramu 74.385
|
|
2.
|
Banghi
(Vifurushi)
|
373
|
|
3.
|
Banghi
(Vifuko)
|
3
|
Natoa wito na tahadhari kwa wananchi wote
wanaohusika kwenye mtandao huu kuacha mara moja kwa kuwa vita hii imeshaanza na
inaendelea kwa lengo la kuhakikisha usalama wa vizazi vilivyopo na vizazi
vijavyo maana madawa haya yanaathiri zaidi vijana ambao ndiyo muhimili na nguvu
kazi ya Taifa.
Aidha nawapongeza wananchi wote waliotoa ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu
huu bila ya kuona muhali. Niwaombe wananchi wote kuendelea na ushirikiano huu
wa kutoa taarifa.
Mwisho natuma salamu kwa watuhumiwa
wote waliotoroka kule walipo wajue kuwa wanatafutwa na watakamatwa ili wahojiwe
na hatimae kufikishwa Mahakamani.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza
Liberatus Sabas – DCP
Mkuu Wa Uperesheni Maalum za Polisi Tanzania
21.03.2018

No comments:
Post a Comment