Habari zilizotufikia hivi punde chumba cha habari cha mtandao huu zinasema kuwa Shule ya Sekondari ya Korigwe Girls iliyoko Korogwe mjini Wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, inaungua moto muda huu. Mpaka tunawaletea habari hii hewani bado haijaweza kufahamika chanzo cha ajali ya moto huo. Kaa nasi hapo baadaye tutawaletea habari kamili.

No comments:
Post a Comment