NYOTA wa
muziki wa dansi nchini, Johnson Nguza maarufu kama ‘Papii Kocha’ anatarajia
kufanya uzinduzi wa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Waambie’ alioutunga
mara tu baada ya kutoka Gerezani kwa msamaha wa Rais.
Mwanamuziki
huyo Papii na baba yake Nguza Viking, walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha
jela ambapo walipata msamaha waRais mnamo Desemba 9, mwaka jana kuachiwa huru.
Uzinduzi huo
uliopewa jina la ‘Viking’ unatarajia kufanyika marchi 10 mwaka huu, katika
Ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam.
Katika
uzinduzi huo pia kutakuwa na wasanii kibao wa muziki wa kizazi kipya
waliothibitisha kumsindikiza Papii, kwa kutambua jitihada zake katika tasnia ya
muziki.
Akizingumza
na mwandishi wa mtandao huu jijini Dar es salaam, msanii huyo alisema anafuraha
kubwa kukutana tena na mashabiki wake na wasanii wenzake katika jukwaa moja
siku hiyo na kuongeza kuwa anaamini siku hiyo itakuwa ni ya kipekee zaidi kwa
upande.
Aliwataja
baadhi ya wasanii waliothibitisha kumsindikiza katika uzinduzi huo kuwa ni
pamoja na Barnaba, Bushoke pamoja na baba yake Nguza Viking.
Uzinduzi huo
utafanyika sambaba na sherehe ya kuzaliwa kwake ili kuwa na maana halisi ya
mimi kuzaliwa upya na kurudi jukwaani rasmi na uhalisia wa jina la wimbo wangu
mpya wa Waambie.
“Nimewamisi
sana mashabiki zangu hata wao wamenimisi pia, nilifurahi jinsi walivyonipokea kilivyopata nafasi ya kuimba japo kwa dakika
chache kwenye shoo ya Mapenzi Mubashara ya Aslay na Nandy, hivyo nimeamua kuzindua
wimbo wangu mpya wa Waambie Siku tarehe yakuzaliwa kwangu ili nipate fursa ya
kufurahi pamoja na mashabiki zabgu”. Amesema
Baada ya
uzinduzi huo mashabiki wa muziki wa dansi watarajie vibao vingine vipya kutoka
kwa Papii ambavyo tayari amekwishaviandaa ili kuwapa raha Watanzania wote
waliommisi katika majukwaa ya burudani.



No comments:
Post a Comment