Dkt. Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)
Kigoma (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega
katikati, kizimba cha kufugia samaki kilichopo katika maji ya ziwa Tanganyika
hakipo pichani, alipotembelea kituo hicho mjini kigoma jana. Kulia ni Afisa
Mifugo wa Mkoa Bw. Noel Byamungu.
Dkt. Emmanuel Sweke Kaimu Mkurugenzi wa kituo wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega aliyekaa katikati wakiwa katika boat wakielekea kuangalia kizimba cha kufugia samaki katika maji ya ziwa Tanganyika, kushoto ni Afisa Mifugo wa Mkoa wa Kigoma Bw. Noel Byamungu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, akizungumza na watumishi wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, pamoja na watafiti hawapo pichani, alipotembelea kituo hicho, kulia ni Dkt Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, na kushoto ni Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo katika chuo cha mafunzo ya uvuvi FETA Kigoma, Bw. Simtie Ambakisye, Naibu Waziri Ulega alifanya ziara katika kituo cha TAFIRI Kigoma pamoja na kutembelea mialo ya Muyobozi na Kibiri.
***************************************
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, amesema kuwa siku za wanaoagiza nyama, maziwa na
samaki kutoka nje ya nchi, zinahesabika kutokana na nchi kuwa na mifigo ya
kutosha kama vile Ngombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku na Punda na hivyo Taifa kama
Tanzania halina sababu yoyote ya kuagiza mazao hayo ya mifugo na uvuvi kutoka
nje ya nchi.
Naibu waziri Ulega aliyasema
hayo alipokuwa katika ziara ya siku tatu Mkoani Kigoma ya kutembelea Mwalo wa
Samaki wa Muyobozi Uliyopo Wilayani Uvinza,Mwalo wa Kibirizi na kituo cha
Taasisi ya Tafiti za Uvuvi Tanzania TAFIRI Kigoma.
“Sioni kwanini tuagize nyama
na maziwa toka nje ya nchi, hatuwezi kuendelea kuangiza nyama,
maziwa na hata mazao ya uvuvi, kwa nini tusiwekeze katika rasilimali zetu za
ndani katika mifugo na samaki na kuongeza
pato la taifa? “Aliuliza Ulega.
Ulega aliongeza kwa kusema kuwa Wizara yake
haitawavumilia waafanyabiashara
wanaoagiza nyama, maziwa na mazao ya samaki toka nje ya nchi kwani sekya ya mifugo na
uvuvi ni sekta ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija katika taifa.
Tarkibani “tani elfu 20 za
samaki zinaingizwa kutoka nje ya nchi kila mwaka, samaki ambao wanafugwa katika
maeneo mengine duniani, lakini sisi hapa nchini tunao katika mazingira ya
asili.” Alisema
Na hapa Mhe. Ulega aliitaka TAFIRI kuhakikisha
wanawafikia wafugaji wa samaki kwa kufanya tafiti zao ili kujua changamoto
wanazokutana nazo na kujua namna ya kuzitatua, akitolea mfano wa chakula sahihi
kinachotakiwa kupewa masamki wanaofugwa na kuangalia miundombinu ya kufugia.
Akizungumzia suala la zana za
uvuvi katika ziwa Tanganyika alipokuwa akiongea na watafiti na watumishi wa
TAFIRI, Ulega alisema
“TAFIRI mfanye tafiti ya aina ya nyavu zinazotumiwa kwa kiasi kikubwa na wavuvi
ili kuona kama zinafaa kuendelea
kutumika, maana kumekuwa na malalamiko toka kwa wavuvi yanayopelekea kushuka
kwa kiwango cha upatikanaji wa samaki na dagaa katika ziwa hili kutokana na
matumizi ya nyavu hizo.” Alisema
Sambamba na hilo Ulega alisema
Wizara yake ina mpango wa kuimarisha eneo la tafiti kwa kuongeza rasilimali
fedha kwa kukarabati miundombinu na kuongeza rasilimali watu.
“Kila Mwaka TAFIRI itakuwa
inafanya tafiti kuhusu mambo ambayo Wizara itakuwa imeyaelekeza ili kuondokana
na suala la watafiti hawa kufanya kazi za watu wengine.” Alisema
Akizungumzia swala la
mafanikio ya soko la nyama la nje ya nchi, Ulega alisema, “Hatuwezi kusafirisha
nyama nje ya nchi kama mkakati wetu wa chanjo ya mifugo hauko sawa, lazima tuwe
na mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mifugo, soko la kimataifa linaangalia sana
swala hili, Sisi kama Wizara tunaenda kusema kuwa kwa yoyote anayetaka kufuga
swala la chanjo ni lazima.” Alisisiza Ulega.
Ulega aliendelea kusema kuwa
ni lazima wizara kutengeneza mikakati ambayo itamfanya mfugaji asitaabike wazo
wambalo amesema kama litaridhiwa litafanyiwa kazi.
“kuna watu wanaona mifugo ni
balaa, mifugo siyo balaa mifugo na neema.” Alisisitiza.
Aidha
Ulega alisisitiza suala la uwekezaji kwa ufugaji wa samaki kama njia ya
kusaidia kupunguza kiwango kikubwa cha uvuvi haramu wa samaki katika maeneo
mbalimbali nchini, huku akipongeza jitihada za taasisi ya utafiti wa samaki
TAFIRI kushirikiana na wananchi na kuonesha mfano wa namna ya ufugaji bora wa
samaki unaowaonesha wafugaji wa samaki kuitumia ili kufikia malengo
waliyokusudia.
Naibu
Waziri Ulega pia alisema Serikali imepanga kuongeza makusanyo katika sekta ya
mifugo kutoka bilioni kumi na sita hadi bilioni hamsini baada ya kuifanya
mifugo ya ndani kuwa bora na kuwa ya kiushindani katika soko la kimataifa, hivyo
suala la chanjo litakuwa la lazima.
No comments:
Post a Comment