Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati akifungua
Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU)
unaohusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi
uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Viwango wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) Dkt. Chauseb Lee kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na ITU kuhusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani uliofanyika Zanzibar
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakati wa mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) uliofanyika Zanzibar kuhusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Dkt. Eng. Maria Sasabo
Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) wa Mawasiliano na Viwango Dkt. Chauseb Lee akifafanua jambo kwa wadau wa TEHAMA wakati wa mkutano wa Nane wa Kijani kuhusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar
Mkurugenzi wa Shirika la
Mawasiliano Duniani (ITU) wa Mawasiliano na Viwango Dkt. Chauseb Lee akifafanua
jambo kwa wadau wa TEHAMA wakati wa mkutano wa Nane wa Kijani kuhusu namna ya
kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa TEHAMA kwenye mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) unaohusu namna ya kutumia TEHAMA kuedana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa Mwamboya akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi James Kilaba wakati wa Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) kuhusu namna ya kutumia TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika Zanzibar. Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Mhandisi Peter Ulanga
************************************************
Wadau wa Shirika la
Mawasiliano Duniani (ITU) wanaohusika na masuala ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) wamekutana Tanzania kutoka nchi mbali mbali duniani kwenye
Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani kwa lengo la kujadiliana namna ya kutumia
TEHAMA kuendana na mabadiliko ya tabia nchi yanaoendelea kutokea duniani.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Makame Mbarawa
amefungua mkutano huo uliofanyika Zanzibar ambao umeandaliwa na Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Mamlaka ya Mawasiiano Tanzania (TCRA) wakiwa
waandaji na wenyeji wa mkutano huo.
Wakati akifungua mkutano
huo, Prof. Mbarawa amewataka wataalamu wote wa TEHAMA kutoka sehemu mbali mbali
duniani kutumia mkutano huo kujadiliana, kuweka mikakati na miongozo ya namna ya
kutumia huduma na bidhaa za TEHAMA kwa maendeleo ya uchumi na viwanda ikiwa ni
pamoja na mbinu za kutabiri na kudhibiti majanga yanayotokea kuendana na
mabadiliko ya tabia nchi kwa kutumia TEHAMA.
Amewataka washiriki wa
mkutano huo kubadilishana uzoefu na kujadiliana namna ya kutumia TEHAMA kulinda
mazingira, kufungua fursa za kiuchumi, kuwa na miji ya kisasa ambayo
inaendeshwa na kusimamiwa kwa kutumia TEHAMA illi kuhakikisha kuwa TEHAMA
inatumika kutunza mazingira ili kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na
mabaki ya vifaa na huduma za TEHAMA na kuweza kurudufu mabaki hayo ii kulinda
usalama wa mazingira na yaweze kutumika kwa matumizi mengine.
Amefafanua kuwa Tanzania
imejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano wenye urefu wa zaidi ya kilomita 25,000
ambao umeunganishwa kwenye taasisi za Serikali na sekta binafsi na kwenye nchi
za jirani ambazo hazijapakana na bahari ambapo umewezeshaji utoaji wa huduma za
mawasiliano nchini ambapo hadi hivi sasa tuna jumla ya watanzania milioni 45 wanaotumia
simu za mkononi, milioni 23 wanaopata huduma ya intaneti na milioni 20
wanaotumia huduma za kielektoniki kama vile kutuma na kupokea pesa, “watu hao
wote wanatumia vifaa mbalimbali vya kielektroniki, baada ya muda vifaa hivi
vitakuwa havifanyi kazi, vimepitwa na wakati, sasa inatakiwa tuvitoe kwenye
soko vizuri bila kuharibu mazingira ambayo tunayatumia, sasa tukikaa hapa na
wataalamu hawa tunaamini tutajifunza njia mbali mbali ambazo zinatumika duniani
katika kuharibu hivi vifaa vya kielektroniki ambavyo vimeshapitwa muda wake”
amesema Prof. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi wa Idara
ya Mawasiliano na Viwango wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU) Dkt. Chaesub Lee amewataka wataalamu hao
kujadiliana na kupeana uzoefu wa kutoka kwenye nchi zao za kutumia fursa za
TEHAMA kuongeza mzunguko wa uchumi na viwanda duniani, kutumia bidhaa na huduma
za TEHAMA kuhifadhi na kulinda mazingira na kuchakata bidhaa na huduma za
mawasiliano ambazo zimepitwa na muda wake au kuharibika ambapo ITU iko tayari
kushirikiana na nchi husika katika nyanja ya utalaamu, ushauri na utekelezaji
wa mipango na mikakati mbalimbali ya namna ya kutumia TEHAMA kuendana na
mabadiliko ya tabia nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika.
Waziri wa Ujenzi,
Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa
Mwamboya wakati akifunga mkutano huo, amewakaribisha washiriki hao kutembelea
vivutio mbali mbali vya kiutalii vilivyopo kwenye visiwa hivyo.
Mkutano huo umeandaliwa
na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania kwa niaba ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
No comments:
Post a Comment