Habari za Punde

MAKUBALIANO YA WAKUU WA NCHI ZA SADC KISWAHILI CHAPIGA BAO

  Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, akiwaongoza marais wa Jumuiya hiyo kusaini mikataba ya Itifaki mbalimbali ya makubaliano wakati wa mkutano Mkuu wa mwisho wa 39 wa Jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, Dk, Stergomena Tax, akisaniana mkataba wa mazingira wezeshi ya Uwekezaji kwenye Viwanda na Balozi wa Umoja wa Ulaya  nchini Botswana, Jan Sadec,  wakati wa mkutano Mkuu wa mwisho wa 39 wa Jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, Dk, Stergomena Tax, akibadilishana mkataba wa mazingira wezeshi ya Uwekezaji kwenye Viwanda na Balozi wa Umoja wa Ulaya  nchini Botswana, Jan Sadec,  wakati wa mkutano Mkuu wa mwisho wa 39 wa Jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, akiagana na Marais wa Jumiya hiyo baada ya kufunga mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.
******************************************
WAKUU wa Nchi na Viongozi wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC)wamepitisha kwa kauli moja lugha ya kuwa lugha rasmi ya nne itakayotumika kwenye jumuiya hiyo.
Kupitishwa kwa lugha hiyo kumetokana na Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo Rais Dk.John Magufuli kuomba lugha hiyo iingizwe kwenye jumuiya hiyo.
Akizungumza leo Agosti 18,2019 kwenye ufungaji wa Mkutano Mkuu wa 39 wa SADC ambao umefanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere Mwenyekiti huyo mpya ametoa taarifa ya kupitishwa kwa lugha ya Kiswahili kuwa rasmi.
"Nianze kutoa hotuba yangu ya kufunga mkutano wa 39 wa SADC kwa kueleza hapa,nilitoa ombi kuhusu lugha ya Kiswahili kutumika kwenye SADC.Wakuu wanachama wameiteua
lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya SADC.
"Narudia tena nawashukuru wakuu wa nchi na wakuu wa Serikali kwa kukubali lugha hiyo iwe rasmi kwenye jumuiya yetu.Baba wa Taifa amekuwa na heshima kubwa sana katika Bara la Afrika.Katika maisha wapo wanajitolea kwa mambo mbalimbali, wapo wanatoa figo,wapo wanaotoa fedha na utoaji wa aina nyingine," amesema.
Amefafanua Mwalim Julius Nyerere yeye aliamua kutoa upendo na maisha yake kwa ajili ya wengine na hivyo sehemu kubwa ya maisha aliyatumia kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa salama na ndio maana nchini Tanzania kuna maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa kambi za wapigania uhuru na hasa nchi za Kusini mwa Afrika. 
 " Mwalimu Nyerere alishiriki kwa vitendo kwa ajili ya kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa huru.Tanzania imekuwa na kambi nyingi za wapigania uhuru na mojawapo ilikuwa eneo la Kongwa ambako anatoka Spika wa Bunge Job Ndugai.
"Namshukuru Rais wa Afrika Kusini kwani ametemblea eneo la Mazimbo mkoani Morogoro ambako kuna makaburi ya mashujaa wa Afrika Kusini.Rais wa Afrika Kusini alikutana na mabinti wawili ambao walikuwa wanamtafuta baba yao,
"Na majina yao yameonekana katika makaburi hayo.Ni uchungu sana lakini kwa sehemu kubwa inaonesha ni namna gani Mwalimu Nyerere aliwapenda wengine," amesema Rais Magufuli.
Amefafanua kwamba wote ambao walikuwa kwenye harakati za kupigania uhuru walikuwa wanatumia lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kuwasaliana.Hivyo ameshukuru lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya nne rasmi ya nne kwenye jumuiya yetu.Mmemfuta machaozi baba wa Taifa.
"Kwa niaba ya Watanzania tunashukuru sana kwa lugha hii kuwa rasmi.Hivyo uamuzi huu wa kuifanya lugha hii kuwa rasmi itainganisha wananchi wetu.Kwa nchi ambazo hawazungumzi Kiswahili, Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kutoa walimu wa somo la Kiswahili kwa ajili ya kuwafundisha wananchi wao," amesema.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.