Habari za Punde

WLAC YAWANOA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI, JIJINI DAR LEO

Wakili Dkt. Cornel Mtaki, akiendesha mafunzo ya siku moja kwa baadhi ya wawakilishi wa Wafanyakazi kutoka Taasisi rasmi na zisizo rasmi ambao ni viongozi wa vyama vya wafanyakazi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo ikiwa ni siku ya kufungwa kwa Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Jamilex Mwenge jijini Dar es Salaam. Mtaki amewataka Viongozi hao kuzingatia maadili pamoja na kufahamu haki za wafanyakazi zinazotakiwa kutimizwa na waajiri wao.
Afisa kutoka WLAC, akifafanua jambo kwa washiriki.Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza kwa makini....Wakili Dkt. Cornrl Mtaki akiendesha mafunzo hayo.

***************************************
Na Nadhifa Muhidin 
*Yahaidi kuwafikia wafanyakazi wengi zaidi na kutoa elimu ya kutambua haki na wajibu katika maeneo yao ya kazi.

KATIKA kuhakikisha wafanyakazi walio katika mifumo rasmi na isiyo rasmi wanapata stahiki zao pamoja na kufahamu majukumu yao ya kazi, Kituo cha msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC,) kimeendelea kutoa mafunzo ya uelewa kwa wafanyakazi ili waweze kufahamu ni nini wanatakiwa kufanya na kufanyiwa na waajiri wao.Afisa Sheria wa kituo cha msaada wa Sheria kwa wanawake (WLAC,) Barcoal Deogratius (kushoto) akiteta jambo na Afisa mwenzake wakati wa mafunzo hayo.
*************************************************************
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa semina maalumu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa sekta rasmi na zisizo rasmi Afisa sheria wa WLAC,, Barcoal Deogratius amesema kumekuwa na wimbi la kutolewa haki na wajibu mahali pa kazi kwa makundi mbalimbali ikiwemo wanawake na watoto.

"Wafanyakazi wengi hawafahamu haki na wajibu wao, Tunaamini kupitia mafunzo haya tunaamini wafanyakazi wa viwandani na sehemu nyingine watafahamu haki na wajibu katika kutekeleza majukumu yao." Ameeleza.

Aidha amesema mradi huo wa miaka miwili umelenga kuwajengea uwezo wanawake na vijana pamoja na waajiri kutambua majukumu yao na kuweza kupunguza migogoro ya sitofahamu na wameanza kwa Mkoa wa Dar es Salaam na baadaye watasambaa katika Mikoa mingine na kutoa elimu hiyo.

Amesema kuwa wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuwafikia walengwa ikiwemo vipeperushi, vyombo vya habari, mawasiliano ya simu na kuwatembelea katika maeneo ya kazi.

"Kupitia njia hizo tumepata mirejesho mingi na mingine kutatuliwa...kikubwa tulichogundua ni uelewa kuhusiana na mikataba, waajiriwa wengi hawana elimu kuhusiana na mikataba ya ajira na mikataba ya huduma (services,) tumelenga kupitia mafunzo haya pamoja na kuwatembelea katika maeneo yao ya kazi tutamaliza tatizo hili linalosababisha migogoro mingi baina ya waajiri na waajiriwa." Amesema.

Vilevile amesema, wamelenga kuwafikia walengwa wapatao Laki tatu kupitia mafunzo pamoja na walengwa wapatao laki tano kupitia njia nyingine za huduma ikiwemo mawasiliano ya simu, vipeperushi na kuwatembelea katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya wanawake ya SBC, watengenezaji wa kinywaji cha Pepsi Swaumu Mkunze amesema kupitia mafunzo hayo wanawake wengi wataimarika zaidi hasa kwa kujua ni nini wafanye na kupata kutoka kwa waajiriwa wao bila aina yoyote ya unyanyasaji.

Amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo, ujaziri, haki na wajibu katika maeneo yao ya kazi na wao kama viongozi watasimama katika kutetea haki za wafanyakazi wao na kuhakikisha waajiri wanatimiza wajibu wao.

"Elimu hii tayari imesaidia kupunguza migogoro mingi katika maeneo ya kazi, awali tulijua tunaonewa kwa sasa tumejua nini tufanye na kipi tufanyiwe tunaimani migogoro baina na waajiri na waajiriwa itakoma." Amesema.

Kituo cha msaada wa sheria kwa Wanawake (WLAC,) kimekuwa msaada hasa kwenye maeneo ambayo bado kuna changamoto kuhusu haki na sheria na inatekeleza majukumu yake kwa Wilaya 23 za Tanzania na kulenga makundi mbalimbali wakiwemo wanawake.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa makini na mada zilizotolewa na waendesha mafunzo ukumbini hapo.Mafunzo yakiendelea
Afisa wa Fedha na Utawala wa TAMICO, Debora Kibona akiwa ni miongozi mwa viongozi waliohudhuria mafunzo hayo.Ufuatiliaji wa mafunzo kwa umakiniUfuatiliaji wa mafunzo kwa umakiniMafunzo hayo pia yalikuwa na mada zilizofurahisha na kuchangamsha...., hapa ni Katibu Msaidizi wa CHODAWU, Agripina Mrosso, akifurahia jambo wakati mtoa mada akiendesha mafunzo hayo.Katibu Msaidizi wa CHODAWU, Agripina Mrosso (kulia) na wenzake wakifuatilia mafunzo hayo kwa umakini.

Mafunzo yakiendelea,.......
Ufuatiliaji ukiendelea.......

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.