Habari za Punde

MBUNGE WA MWERA AANZA KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI, AZINDUA UJENZI WA BARABARA YA GARAGARA MTONI KIDATU

MWENYEKITI wa CCM Jimbo la Mwera, Mohamed Ameir Makame (katikati) akiwainua mikono Mbunge wa jimbo hilo, Zahor Mohammed Haji na Mwakilishi wake, Mihayo S. Juma Nh'unga, ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi kuanza kwa ujenzi wa Barabaa ya Garagara Mtoni Kidatu yenye urefu wa Kilometa tatu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ulioanza leo, katika jimbo hilo eneo la Mtoni Kidatu mjini Zanzibar. (Picha na Muhidin Sufiani)
Mbunge Zahor akipanda katika Katapila kuanza kazi hiyo ya ubomoaji...
MBUNGE wa Jimbo la Mwera, Zahor Mohammed Haji, akitoa maelekezo wakati wa zoezi la ubomoaji nyumba zilizojengwa eneo la barabara ili kupisha ujenzi wa Barabara ya Garagara Mtoni Kidatu yenye urefu wa Kilometa tatu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ulioanza leo, katika jimbo hilo eneo la Mtoni Kidatu mjini Zanzibar. 
Kazi ya ubomoaji ikiendelea.................
Wakazi wa Eneo hilo wakishuhudia zoezi la ubomoaji
Jino kwa jino hadi kieleweke....................
Ukaguzi wa kazi ukiendelea.....................
SHEHA wa Shehia ya Jimbo la Mwera, Rashid Jadi Rashid, (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) na baadhi ya viongozi  wa CCM wa Jimbo hilo wakati wa  hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Garagara Mtoni Kidatu, uliozinduzliwa leo/

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.