Habari za Punde

WLAC WATOA MAFUNZO KWA WAFANYAKAZI, CHAMA CHA WAAJILI, WALIMU, MASHIRIKA NA TAASISI

Mwanasheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mathew Ngaga, akiendesha mafunzo ya Haki za Wafanyakazi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikumi, Hoteli ya Jamilex leo na kushirikisha baadhi ya mashirika na Taasisi mbalimbali nchini.
***********************************
Na Nasma Kalonga
Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Mwanasheria wa Kituo cha msaada wa sheria kwa Wanawake WLAC na mratibu wa mradi wa Uwezeshaji Jamii katika Masuala ya Haki na sheria za Ajira, Consolata Chikoti, amesema kuwa wamewakutanisha walimu pamoja na wafanyakazi wengine kutoka Taasisi na Mashirika mengine ili kwa pamoja waweze kujua na kuzitambua haki na sheria ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo ili waweze kusaidia kusimamia haki za wafanyakazi katika mashirika, Taasisi mbalimbali na Vyama vya wafanyakazi.
''Lengo la mafunzo haya ni kuona namna ya kukutana na kujadili kwa pamoja jinsi ya kuwasaidia wafanyakazi na kuwaongezea uwezo katika maeneo muhimu na ya msingi maeneo yao ya kazi ili waweze kusimamia haki za wafayanakazi ipasavyo''. amesema Chikoti
Aidha Chikoti amesema kuwa Kituo cha WLAC kimefanya mafunzo hayo baada ya kugundua kuwa kuna changamoto nyingi katika maeneo mbalimbali ya kazi ambapo hukosa uwajibikaji na kuhakikisha kuwa sheria hizi za kazi zikitekelezwa ipasavyo.
Chikoti aliwaasa waajili kuangalia zaidi maslahi, haki na usalama wa wafanyakazi makazini yanazingatiwa ipasavyo. 
Naye, Katibu wa Chama cha walimu Manispaa ya Ilala, Vicky Kibona, ameishukuru WLAC kwa kundaa mafunzo hayo ambayo yameongeza uelewa kwa wafanyakazi na kujifunza sheria za msingi kuhusu mwajili na mwajiliwa ambao wanatakiwa kufuata sheria na utaratibu endapo wanahitaji kuvunja mkataba, na kuongeza kuwa kumekuwepoa na kesi nyingi za waajili kuwaachisha kazi wafanyakzi bila kufuata utaratibu kutokana na kutojua sheria ama kufuata utaratibu. 
Baadhi ya washiri wa mafunzo hayo wakisikiliza kwa makini kinachoelezwa na waendesha mafunzo ukumbini hapo.
Chikoti akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wakisikiliza kwa makini 
Katika mafunzo hayo pia suala zima la afya lilizingatiwa kikamilifu kwa kugawa Barakoa kwa washiriki kabla ya kuanza kwa mafunzo.
Mafunzo  yakiendelea...........

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.