Habari za Punde

NBC YAIPIGA TAFU ROTARY CLUB KUKUSANYA FEDHA MILIONI 44 ZA SHULE YA MTAKUJA


KATIKA Kuunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Sekta ya elimu, Benki ya NBC imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Taasisi mbalimbali ili kusadia jamii.

Benki ya NBC imeungana na Rotary Club Bahari Tanzania kukusanya fedha kiasi cha Shillingi Milion 44 ili kusaidia Shule ya Sekondari Mtakuja.

Fedha hizo zimekusanywa kupitia Mashindano ya mchezo wa Golf yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana Jijini Dar es Salam

Akizungumzia ushiriki wao kwa mwaka wa tatu mfululizo, Mkurugenzi wa Wateja wa Kati NBC Moses Minja amesema wamekuwa katika ushiriki wa ukusanyaji huo wa fedha kwa ajili ya kusaidia Shule ya Mtakuja kwa kipindi cha miaka mitatau.

Minja amesema, NBC imelenga katika kusaidia jamii na hilo wanalifanya ili kuunga mkono juhudu za serikali za kuinua sekta ya elimu Tanzania.

“Tumekuwa na ushirikiano na Rotary Club kwa miaka mitatu, NBC utaratibu wetu ni kuisaidia jamii na hili tunalifanya kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali,”

“Leo tupo hapa katika Viwanja vya Gymkhana na Klabu ya Rotary kwa pamoja kuweza kukusanya fedha zitakazosaidia Shule ya Mtakuja na hatutaishia hapa bali tutaendelea kila mwaka,”

Kwa upande wa Rais wa Rotary Club Bahari Tanzania Diamond Carvalho amesema Wamekusanya jumla milion 44 kutoka kwa wadhamini mbalimbali waliojitokeza ikiwemo Benki ya NBC.

Carvalho amesema, Rotary wamekuwa na utaratibu wa kutoa kwa jamii na Katika shule ya Mtakuja wameshirikiana nao kwa miaka 11 wakianzia ujenzi wa madarasa, Maktaba, Kisima cha Maji na kwa mwaka huu wana mpango wa kuwanunualia wasichana taulo za kike ili kuwasaidia kutokukaa nyumbani na kuendelea na shule.

Aidha, amewaomba wadhamini wengine kujitokeza ili kuzidi kuzisaifia shule zingine zaidi na Rotary Tanzania wana mpango wa kwenda katika shile zingine.

Benki ya NBC imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu.

Katika mashindnao hayo ya Golf
Mshindi wa Jumla ni David Jansen (40points)
Runner Up: Xiho Long (40points)
Mshindi kwa wanaume (Mens): Amandeep Dhani (40 points)
Runner up (Mens): jiten Lavingia (38 points)
Mshindi kwa wana wake (Ladies): Yvonne Ondari (38 points)
Runner up (Ladies): Jing Sun (37 points)
Mshindi wa nje: Sam Kileo (36 points)
Mkwaju Mrefu wanaume: Taha Jabir
Mkwaju mrefu wana wake: Tayana William
Aliyepiga karibu zaidi ni Alfred Kinswaga
Zawadi ya aliyeandaa mashindano: Kiki Ayonga
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya mchezo wa Golf yakishirikisha taasisi mbalimbali kwa ajili ukusanya fedha ili kusaidia Shule ya Sekondari Mtakuja. Mashindano hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana Jijini Dar es Salam
Caption: Rais wa Rotary Club Bahari Tanzania Diamond Carvalho (kulia) akimpatia cheti cha Ushiriki Mkurugenzi wa Wateja wa Kati NBC Moses Minja wakati wa Mashindano ya Mchezo wa Golf ili kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia Shule ya Sekondari Mtakuja.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.