Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mkuu wa JKT Brigedia
Jenerali Rajabu Mabele (kushoto) pamoja na mkuu wa kikosi namba 834 JKT Makutupora Dodoma, Luteni Kanali
Festo Mbanga (kulia) wakati alipokuwa akitoa maagizo ya upandaji miti pembezoni mwa barabara ya kuingia jiji la
Dodoma leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitembelea na kukagua upandaji miti eneo la pembezoni mwa barabara ya kuingia mkoani Dodoma iliopo JKT Makutupora leo.*******************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewataka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Kikosi namba 834 Makutupora kilichopo
mkoani Dodoma kupanda miti pembezoni mwa barabara ya kuingia jiji la Dodoma ili
kuhifadhi mazingira pamoja na kupendezesha eneo hilo.
Makamu wa Rais amesema hayo alipotembelea
eneo hilo la JKT Makutupora ambapo amesisitiza uwepo wa kambi hiyo ya jeshi
katika eneo hilo ni kwa sababu ya ulinzi wa chanzo cha maji katika bonde la
mzakwe hivyo wanapaswa kufanya uhifadhi huo kikamilifu.
Aidha Makamu wa Rais amewataka JKT
Makutupora kuhakikisha wanadhibiti waharibifu wa mazingira na waoingiza mifugo
na kuchoma mkaa jirani na chanzo cha maji mzakwe. Amesema serikali
imeweka mkazo katika uhifadhi wa mazingira na tayari imeleekeza upandaji miti
katika ngazi za kaya ambapo kila kaya inapaswa kupanda miti mitatu hadi mitano
kulingana na maeneo husika.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajabu Mabele amesema JKT itatekeleza kikamilifu
maagizo hayo na kuweka mkazo katika uhifadhi wa eneo hilo na sehemu zinginezo
zinazohusika na JKT.
No comments:
Post a Comment