Habari za Punde

KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI WAKAZI WA DAR WACHANGAMKIA FURSA UPIMAJI AFYA BURE

Mpimaji wa Maabara kutoka Zomola Specialized Polyclinic, Gladness Hamza, akimpima, Hadija Mtwana, kati ya wakazi wa Dar es Salaam, waliojitokeza kupima afya katika viwanja vya Leaders.
Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam, wakiwa katika foleni ya kusubiri kupata huduma ya kupima.
Na Raul Omary
Kituo cha Redio cha E FM kwa kushirikiana na baadhi ya mashirika na makampuni ya watu binafsi , leo kwa pamoja wameweza kuwakutanisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam na kutoa huduma za upimaji magonjwa ya Saratani, macho na mengineyo bure.
Wakazi hao kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na viunga  vyake wamejitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Leaders leo kwa ajili ya kuapata huduma hiyo iliyotangazwa kutolewa bure kwa  siku mbili mfululizo.
Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa zoezi hilo kutoka Kituo cha Redio na Tv E FM, Swebe Santana, amesema kuwa kuelekea kilele cha Siku ya Mwanamke Duniani inayoadhimishwa tarehe 8 ya mwezi machi kila mwaka, wameona ni bora kumkumbuka mwanamke na kumtukuza kwa kumpa huduma ya kupima maradhi hayo ili ajitambue na kupata matibabu ama ushauri Zaidi kutoka kwa madaktari.
Aidha amesema kuwa anashukuru kuona wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakijitokeza kwa wingi na hiyo ni kuonyesha kuwa maradhi hayo yaliyotangazwa yapo na yanawasumbua kina mama na baadhi ya kina baba waliojitokeza na wengi wao wakishindwa kumudu gharama za matibabu.
“Kwa uitikio huu ni dhahiri kuwa wananchi wengi wana matatizo na wengi wanashindwa kumudu gharama za matibabu na kutenga muda wao kwa ajili ya kucheki afya zao, kwa kuliona hili E FM tumeona ni bora kujitoa kwa wananchi na kuonyesha umuhimu wa kujua afya kwa kutoa huduma bure kwa siku mbili mfululizo ambapo tumeshirikiana na baadhi ya Makampuni wambao pia wameitikia wito na kujitoa kuwasaidia wananchi” amesema Swebe
Swebe alitoa shukrani kwa baadhi ya Makambpuni na mashirika yaliyoshirikiana na E FM kufanikisha jambo hilo ambayo miongoni mwao ni pamoja na Zomola Specialized Polyclinic, Aga Khan Hospital, DSTV, Coca Cola, Assemble Insurance, Vodacom na mashirika mengine.
Wananchi walio jitokeza kupata huduma hiyo katika viwanja vya Leaders Club leo, foleni kubwa hasa ilikuwa ni katika upimaji wa Saratani, Macho na Kisukari.
mafoto media iliweza kufika katika eneo husika nakuwaoji watu mbalimbali wakiwemo viongozi, madaktari,wagonjwa waliotokea maeneo hayo.
Aidha Swabe alisema kuwa  zoezi hilo la upimaji llitakuwa ni endelevu ambapo baada ya kukfanyika jijini Dar es Salaam, pia litafanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ili kufikisha ujumbe kwa wananchi kuwa na utaratibu wa kupima afya na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 8 mkoani Dodoma ili kupima afya ambapo itakuwa ndiyo kilele cha siku ya Mwanamke.
Naye Daktari wa macho kutoka Focus Optionetry Clinic iliyopo Kisutu Dar es Salaam, Salome Urasa, alisema anashukuru kuona uitikio wa wananchi katika zoezi hilo na kuongeza kuwa wao kama Madaktari wametimiza wajibu wao katika kuwahudumia na kujua matatizo na kutafuta masuluhisho kwa kuwatibia, kuwapatia dawa kwa wale waliokuwa na matatizo madogo madogo na wengine kuwapa ushauri nini cha kufanya ili kupata matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.