Habari za Punde

SERIKALI KURUHUSU TRENI ZA WAWEKEZAJI BINAFSI MRADI WA SGR

,
NA MUHIDIN SUFIANI, Dodoma
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amesema serikali inakusudia kufanya mabadiliko ya Sheria ya Reli kwenye bunge lijalo kuruhusu sekta binafsi kutoa huduma na kuleta ushindani katika sekta hiyo kibiashara
Hayo yamesema jana wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kutembelea na kukagua mradi wa Reli ya Kisasa ya Umeme ya SGR kipande cha Morogoro hadi Makutupola.
"Tunategemea bunge la mwezi wa Machi, Aprili hadi Mwezi wa 6 tupitishe Sheria itakayoruhusu hata sekta binafsi waweze kuwekeza katika Reli yetu, kwa maana ya kuwa na return envestment, kwani thamani ya mradi ni trilioni 23 ili iweze kurudi ni kuruhusu wawekezaji bunafsi kuleta vichwa vyao vya treni, watakaoleta mabehewa yao ili iwe kama mfumo wa barabara unavyotunika," alisema
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, Seleman Kakoso, alisema kama kamati wapo tayari kusapoti bungeni mpango huo katika mabadiliko yatakayofanyika katika sekta hiyo.
"Napenda kuwahakikishia serikali tupo tayari kushirikiana nao kufanya mabadiliko haya makubwa ili kuhakikisha ushiriki kamili wa sekta binafsi ili kupunguza gharama na kurudisha gharama ya uwekezaji mkubwa uliofanyika chini ya Rais Samia Suluhu," alisema
Kakoso, alisema kumekuwa na ucheleweshaji wa ukamilishaji wa miradi ya SGR kwa sababu zisizokuwa na ushawishi hivyo kupoteza muda mwingi wa utekelezaji na seriksli kushindwa kutimiza makengo Yao.
"Watu wanataka kuona miradi inakamilika kwa wakati na waweze kufanya shughuli zao za kimaendeleo, ili kwetu liwe somo na kusitokee kucheleweshwaji wa miradi mingine na kuichonganisha serikali na wananchi.
Kaimu Mkurugenzi wa Ishara, Mawasiliano na Umeme wa Shirika la Reli Tanzania, Mhandisi Mateshi Titto, (mwenye kipaza sauti) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wakiwa katika Kituo kikubwa cha Stesheni kilichopo eneo la Kikuyu nje kidogo ya Jiji la Dodoma, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Kakoso (kulia kwake) wakati wa ziara ya Wabunge hao kukagua mradi wa SGR kutoka jijini Dodoma hadi Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu na Ujenzi wa Shirika la Reli Tanzania, Eng. Machibya Masanja (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiwa katika Kituo kikubwa cha Stesheni kilichopo eneo la Kikuyu nje kidogo ya Jiji la Dodoma, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Seleman Kakoso (katikati) na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete (kushoto kwake) wakati wa ziara ya Wabunge hao kukagua mradi wa SGR kutoka jijini Dodoma hadi Morogoro. (Picha na Muhidin Sufiani)
Kituo Kikuu cha Stesheni ya Treni ya Umeme SGR kilichojengwa Kikuyu nje kidogo ya Jiji la |Dodoma kikiwa katika hatua za mwishi za marekebesho.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.