Habari za Punde

*MGAMBO WAKAMATA BIASHARA ZA MACHINGA, WAPAKIA KWENYE 110, WAONDOKA NAZO.

Mgambo wa Manispaa ya Ilala wakipakia maji waliyowanyang'anya wafanyabiashara katika Kituo cha daladala cha Akiba Dar es Salaam leo. Pamoja na kauli ya Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, kuwataka mgambo hao kutowapora biashara zao wamachinga, lakini Mgambo hao wanaonekana kupuuza agizo hilo ambapo siku hizi mgambo hao wamekuwa wakifanya kama mradi kwani wamekuwa wakibeba mabegi kwa ajili ya kuweka biashara wanazowapora Chinga na kutokomea nazo bila kufikisha mahala husika.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.