Habari za Punde

*ZANTEL IMEJIPANGA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI, YADHAMINI UJIO WA MPIRA MAALUM WA KOMBE LA DUNIA

Meneja Masoko wa Zantel Bw. William Mpinga akitoa hotuba kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel kwenye sherehe za kuukaribisha rasmi mpira maalum wa kombe la dunia iliofanyika leo katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam. Zantel ndio wadhamini wakuu wa ziara ya
mpira huo hapa nchini, kwa kushirikiana na baadhi ya makambpuni ya nchini.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera (katikati) akitia saini kwenye mpira uliosafiri kutoka nchini London na kupitia Tanzania ukielekea nchini Afrika ya Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia, ambako utatumika kuzindua mashindano hayo, wakati wa hafla ya kutia saini mpira huo na kuukaribisha iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Spirit of Football 'The Ball', Christian Wach (kulia) ni Meneja Masoko wa Zantel, ambao ni miongoni mwa wadhamini wa ujio huo wa mpira, William Mpinga.

Meneja Masoko wa Zantel Bw. William Mpinga naye akiweka saini yake kwenye mpira huo maalum wa kombe la dunia kwa niaba ya Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa ziara ya mpira huo nchini Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Spirit of Football, Andrew Aris.

Huyu si mwingine ni msanii mahiri wa kughani mashahiri, Mrisho Mpoto naye pia akitia saini katika mpira huo.

"Hata mie naweza bwana Maximo alinibania tuuu alipokuja kuuule naniliu"
Ebwana eeh! kumbe Maximo hapati tu muda wa kutembea na kutafuta vipaji vingine, jaama yumo bwana, Emillian Rwejuna wa Kampuni ya Precisionair, ambao pia ni miongoni mwa wadhamini wa ujio wa mpira huo, naye akionyesha umahiri wake kwa kuucheza mpira huo kwa staili ya kupiga 'Control'.

"Ebwana eeeh! kumbe mgumu namna hii duh!"
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, akiruka kupiga kichwa mpira huo baada ya kurushiwa na mmoja wa viongozi wa msafara wa mpira huo.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera akipiga danadana mpira huo uliosafiri kutoka nchini London na kupitia Tanzania ukielekea nchini Afrika ya Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia, wakati wa hafla ya kutia saini na kuukaribisha mpira huo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam leo.

Ebwana eeh! kumbe si fani ya picha pekee hata soka limo kwa Sufianimafoto, aliyewawakilisha waandishi wenzake wa habari kutia saini katika mpira huo na kama ilivyo ada ya mpira huo kabla ya kutia saini ni lazima uonyeshe uwezo wako katika kuuchezea kwa namna yeyote ile na ndivyo Sufianimafoto alivyofanya kama anavyoonekana pichani.
No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.