Hii ndiyo Kamati ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Taswa ya Maandalizi ya shughuli hii ya kutoa Tunzo kwa wanamichezo bora wa mwaka 2009, ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Hawa ni wanamichezo bora waliofanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro cha tatu bora ili kumsaka Mwanamichezo Bora wa mwaka. Kutoka (kushoto) Mchezaji wa netiboli wa timu ya JKT Mbweni, Mwanaidi Hassan, Kipa wa simba ya jijini Dar es Salaam, Juma Kaseja na mnyanyua vitu vizito, David Nyombo, wakiwa jukwaani wakati wakisubiri hatua ya kutangazwa mshindi wa kwanza kati yao.
Kilio cha Furaha, Machozi ya Furaha....!
Mwanaidi Hassan, akilia kwa furaha baada ya kutangazwa kutwaa tunzo ya Taswa ya mwaka 2009, baada ya kupata pointi nyingi zaidi katika kura zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo.
Kilio cha Furaha, Machozi ya Furaha....!
Mwanaidi Hassan, akilia kwa furaha baada ya kutangazwa kutwaa tunzo ya Taswa ya mwaka 2009, baada ya kupata pointi nyingi zaidi katika kura zilizopigwa na waandishi wa habari za michezo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Idd Kipingu, akimkabidhi Tunzo mchezaji Bora wa jumla wa mwaka 2009, Mwanaid Hassan, aliyekuwa mfungaji bora wa mabao katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati iliyofanyika Kigali Rwanda, ambapo Mwanaidi alifunga jumla ya mabao 275 akiwa na timu yake ya JKT Mbweni, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Mwanaidi akikabidhiwa Mfano wa Hundi ya Shilingi milioni 1
Mwanaidi akirejea kwenye siti yake baada ya kunyakua zawadi za Taswa.
Juma Kaseja akikatiza katikati ya waandishi wa habari na wageni waalikwa kuelekea jukaani.
Mwanaidi akirejea kwenye siti yake baada ya kunyakua zawadi za Taswa.
Juma Kaseja akikatiza katikati ya waandishi wa habari na wageni waalikwa kuelekea jukaani.
Mgeni Rasmi, Idd Kipingu akipiga picha ya kumbukumbi na wachezaji waliokabidhiwa tuzo, wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi.
Wasanii wa kikundi cha Sanaa cha Wanne Star, wakionyesha umahiri wao jukwaani wa kujikunja kwa mtindo wa sarakasi wakati wa sherehe hizo.
Mtangazaji wa redio Tumaini, Domina Rwemanyila, akimkabidhi Tunzo, bingwa wa kunyanyua vitu vizito, David Nyombo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania, George John, akimkabidhi Tunzo, Abdallah Saleh, kwa niaba ya golikipa, Mohamed Mwarami.
Mwandishi wa habari wa Televisheni ya Taifa TBC1, Angela Msangi, akimkabidhi Tunzo, Bondia Francis Cheka, aliyeibuka kidedea baada ya kumchapa Japhet Kaseba mwaka jana.
Mhariri wa gazeti la Spot Starehe. Masoud Saanani, (kushoto) akimkabidi Tunzo ya mfungaji bora wa mabao John Boko, aliyeongoza kwa magoli mwezi Septemba 2009.
Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo cha redio cha Uhuru, Angel Akilimali, akimkabidhi Tunzo, mchezaji bora wa Tenesi wa timu ya watoto, Shaban Ibrahim, aliyeiwezesha timu yake kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Afrika mwaka 2009.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Leo Juma Pinto, (kushoto) akimkabidhi Tuzo mwanamichezo bora wa mwezi Julai 2009, Mohamed Abdulrahim, aliyekuwa mfungaji bora wa mabao katika michuano ya Copa Cocacola.
Mchora Katuni mahiri ya Baba Tau, Adam Rutta ‘BABA TAU’, akimkabidhi tuzo mwanariadha Banwelia Bryton, aliyeshinda mbio za Half Marathon zilizofanyika Kigali Rwanda mwaka 2009.
Meneja wa mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy mapunda, akimkabidhi Tunzo, Mwanaidi Hassan. Kulia ni Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Mgaya Kingoba.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia Serengeti, Mark Bomani, akimkabidhi tuzo, golikipa wa Simba, Juma Kaseja, aliyeibuka mchezaji bora wa mwaka 2009, wakati akiwa na timu ya Yanga, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari za Michezo Taswa, kilichoratibu Tuzo hizo, Boniface Wambura (kulia) ni Katibu wa Chama hicho, Mgaya Kingoba
Hawa si Mamisi bali ni warembo wa fild uandishi wa Habari, wakipozi kwa picha yaani haya ndiyo maua ya News room zetu jamani au siyo????
Baada ya zoezi zima la kukabidhi zawadi kilichofuata ilikuwa ni mpango mzima wa masuala ya maakuli, kama unavyocheki meza ilivyosheheni huku kila mmoja akiwa bize na kisu na umma...
Hii ilikuwa ni meza ya wachezaji walioalikwa katika shughuli hiyo ambao baadhi yao ndiyo hasa walioibuka na tuzo hizo za Taswa..., hapa ni wakati wakijisevia maakuli.
Wakati wa kula hakuna kulemba, Ubrazamen wala Usistaduh, kama unavyocheki hapa kila mmoja akiwa bize.....
Huyu ni mmoja kati ya wapishi walioandaa msosi huo, hapa akiandaa meza ya matunda....
Wageni waalikwa Wanamichezo na waandishi wakijisevia msosi..
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za michezo Tanzania (TASWA), Boniface Wambura, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Wanamuziki wa bendi ya Karunde, wakitumbuiza jukwaani wakati wa haafla ya Chama cha waandishi wa habari za michezo Taswa, ya kukabidhi zawadi za wanamichezo bora wa 2009, iliyofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam jana usiku, na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Serengeti, Teddy Mapunda (katikati) akiwa na wageni waalikwa.
Kutoka (kushoto) Ally Mkongwe A.K.A Teacher akiwa na Mwani Nyangassa na Ellius Kambili, wakisebeneke na Biereeeee, hapa ilikuwa haina kulemba katika suala zima la kumnaniliu mnyama 'CHUI'............
Hii ilikuwa ni meza ya wahariri kama unavyoicheki ilivyotulia haina shobo.
Mhariri wa gazeti la Bingwa Grace Hoka, akiwa na Mhariri wa gazeti la Habari Leo, wakati wa hafla hiyo.
'SEBENE LA ALADJI'
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda akisakata rhumba ‘Aladji’ na mtangazaji wa televisheni ya Star Tv, Tom Chilala, aliyekuwa mshereheshaji wa sherehe hiyo, hapa ndo ilikuwa mwishooooooooo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda akisakata rhumba ‘Aladji’ na mtangazaji wa televisheni ya Star Tv, Tom Chilala, aliyekuwa mshereheshaji wa sherehe hiyo, hapa ndo ilikuwa mwishooooooooo.
No comments:
Post a Comment