Rais wa Shirikisho la Kabumbu nchini, Leodger Tenga, akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya timu za Taifa Stars, Brazil na Twiga Stars, kusambaza ujumbe wa Malaria katika nchi 160 ili kutokomeza ugonjwa wa Malaria. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Moven Pick jijini Dar es Salaam jana.
Waziri wa Kazi, Ajila na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma kapuya, akiteta jambo na Mkuu wa Msafara wa timu ya Brazil, Andres Sanchez, wakati wa hafla hiyo.
Profesa Juma Kapuya, akisalimiana na wachezaji wa Twiga Stars, wakati wakiingia kwenye hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa CECAFA, Nocolas Musonye (kushoto) akiteta jambo na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda, ambao pia ni wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa Stars.
Teddy Mapunda akipozi kwa picha na baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars.
No comments:
Post a Comment