Wapiga Picha za Habari wa vyombo tofauti, wakiwa getini wakisubiri ruhusa ya kuingia Uwanja wa taifa ili kuendelea na kazi ya kupiga picha katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya Taifa Stars na Brazil, baada ya kuzuiliwa kuingia japo kila mmoja alikuwa na tiketi yake mkononi na vifaa vya kufanyia kazi. Askari hao waliowazuia waandishi hao walidai kuwa hawakupata maelekezo yeyote kutoka kwa wahusika kuhusiana na wapiga picha wanaotakiwa kuingia ndani ya uwanja huo kwa ajili ya kupiga picha, jambo ambalo lilimkera kila mmoja na kuwa kero ya kila siku na usumbufu ambao hadi leo hauna muafaka, kwani waandishi na wapiga picha wamekuwa wakitumiwa vibaya pale tu kufanya kazi lakini inapofikia suala la kuwajali hakuna anayekumbuka fadhila angalau basi kwa kuwaandalia mazingira mazuri ya kufanyia kazi yasiyokuwa na usumbufu. Hili lkinawezekana tena sana tu iwapo wahusika watawapa kipaumbele watu hawa wanaowatangazia kazi zao za kila siku, ama urafiki ushirikiano ni pale tu wanapokutana TFF????????, WAHUSIKA FANYIENI KAZI JAMBO HILI VINGINEVYO IPO SIKU HAKUNA ATAKAYEANDIKA KAZI ZENU.....
Kikosi cha Brazil katika picha kabla ya kuanza kwa mtanange huo, kwenye Uwanja wa Taifa jana.
Brazil....na watoto...
Rais Jakaya kikwete, (watatu kushoto), Rais wa shirikisho la Soka nchini TFF, Leodger Tenga (wapili kushoto), Katibu Mkuu wa CECAFA, Musonye (wanne kushoto) na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wakati ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Rais Jakaya akisalimiana na wachezaji wa Brazil......
Rais Jakaya akisalimiani na Robinho......
Rais Jakaya akisalimiana na Nizar Khalfan......
Picha ya kumbukumbu....
Mchezaji wa Taifa Stars, Mussa Hassan Mgosi akimtoka beki wa Brazil, Michael Bastos, wakazti wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Brazil ilishinda kwa mabao 5-1, bao la Taifa Stars lilifunngwa kwa kichwa na Jabr Aziz aliyengia sabu kipindi cha pili dakika ya 86.
Wachezaji wa taifa Stars, wakichuana na wa Brazil wakati wakisubiri mpira wa kona upigwe....
Mrisho Ngassa, akimnyanyasa, Robonho, hapa ni baada ya kumpiga chenga na kumtoka na kisha kupiga krosi matata iliyomkta Kigi Makasi na kupiga fyongo mpira huo.....
Huu ulikuwa ni muda wa mapumziko, Mwandishi wa habari za michezo wa ITV na Redio One, Farouk Kharim, akipiga picha ya kumbukumbu na Kaka.......
Robinho wa Tanzania, Uhuru Selemani, akimpa mpira Robinho ili aweke saini wakati wa mapumziko....
Kocha wa Brazil, Dunga, akiweka saini katika mpira aliopewa na Nahodha wa taifa Stars, Shadrack Nsajigwa....
Mfungaji wa bao la kufutia machozi, Jabir Aziz, akipiga picha ya kumbukumbu na Thiago Silva wa Brazil, baada ya kuweka saini katika mpira wake....
Ebwana katika mechi hii nilijifunza mengi kuhusiana na wenzetu wanavyofanya kazi.....ama kweli sisi hapa home tunacheza,...jamani hivi vijikamera vyetu nadhani ni vya Bathidei tu jamani, hebu cheki jamaa walivyokuwa bize... hivi ndivyo wanavyofanya kazi wenzetu wa duniani....
Humoud akichuana na Kaka........
Robinho, akijiandaa kumtoka beki wa Stars, Stephano Mwasika....
Kipa wa Strs Mwarami. akihaha tu bila kujua la kufanya langoni kwake, wakati ulipopigwa mpira wa krosi...
Beki wa Stars, Kelvin Yondan, akimsindikiza mshambuliajiwa Brazil, Ramires, aliyemshinda na kupiga shuti lililomshinda kipa wa Stars Mwarami na kutinga wavuni na kuandika bao la nne kipindi cha pili.....
Ebwana eeh! hii ilikuwa ni kali ya mwaka kwa upande wa Tanzania, Jamaa huyu aliibukia tu katikati ya Uwanja akishangilia baada ya kufanikiwa kumkumbatia mchezaji wa Brazil, Kaka wakati mchezo huo ukiendelea. Jamaa huyo alisikika akisema jukwaani wakati akiwa na wenzake kuwa "Leo sikubali hadi nimguse Kaka nitapata hela tu, ila nasubiri askari akigeuka tu nakwenda" alisema jamaa huyo aliyetambulika kwa jina la Ally Komba ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Green Acres ya jijini Dar es Salaam, na ndivyo alivyofanya kwani alianza kwa kuvua viatu na kuviacha jukwaani na kisha kuruka uzio na kisha kukimbia kueleke katikati ya uwanja hadi alipofanikiwa kumkumbatia Kaka, hali iliyomfanya Kaka kubaki na alama ya kuuliza hadi alipomuelewa lengo lake na kuamua kumpa dole, basi jamaa litoka hapo akishangilia kuelekea nje ya uwanja na kudakwa na polisi wetu waliokuwa wamezubaa wakiangalia soka badala ya usalama.
"MMECHELEWA NIMESHATIMIZA AZMA YANGU KUMGUSA TU KAKA".
Askari Polisi wakimdhibiti kijana aliyetambulika kwa jina la Ally Komba, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Green Acres ya jijini Dar es Salaam, baada ya kuvamia katikati ya uwanja na kumkumbatia mchezaji wa Brazil, Ricardo Da Santos Kaka, wakati mchezo ukiendelea, na kisha kutoka akiwa na furaha huku akishangilia baada ya kutimiza azma yake hiyo. Hata hivyo mashabiki wa soka wamelaani kitendo cha askari wanaokuwa na jukumu la ulinzi uwanjani hapo kwa kuacha kulinda usalama badala yake kuwa bize na kuangalia soka.
Kaka, akirajibu kukatiza kwenye msitu wa mabeki wa Stars....
Beki wa Stars, Kelvin Yondan, akionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya, Luis Fabiano....
Kipa wa Stars, Mwarami akiwa hoi chini baada ya kushindwa kuokoa mpira aliopigwa langoni kwake....
Canavaro (kushoto) akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Brazil....
"Hapa hupiti weweeeeeeee"
"Hapa hupiti weweeeeeeee"
Canavaro akimdhibiti mchezaji wa Brazil, Daniel Alves (katikati) ni Uhuru Seleman....
Daniel Alves, akimkandamiza Uhuru Seleman chini baada ya kushindana kwa ubavu na kisha kumnaniliu na kiwiko.....
Ebwana washkaji kweli wamekuja kazini.......
Kocha wa Brazil Dunga, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
"TUNAOMBA UKAWE BALOZI WETU HUKO BRAZIL"
Rais Jakaya Kikwete (katikati) akimkabidhi zawadi ya kinyago mchezaji wa timu ya Taifa ya Brazil, Ricardo Da Santos Kaka, baada ya kumalizi kwa mchezo wa kirafiki wa Kimataifa wa Taifa Stars na Brazil, uliochezwa kwenye Uwanja wa taifa Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment