Habari za Punde

*JENGO LA WIZARA YA ARDHI LANUSURIKA KUWAKA MOTO LEO

Baadhi ya wafanyakazi wa kwenye jengo la Wizara ya Ardhi, wakiwa nje ya jengo hilo leo asubuhi baada ya kutokea shoti ya umeme kwenye moja ya chumba cha jengo hilo na kusababisha mtafaruku mkubwa baada ya wafanyakazi hao kuona moshi ukitoka kwa wingi ndani ya chumba hicho kilichopo chini. Imeelezwa kuwa shoti hiyo imetokana na nyaya za umeme zilizokaa bila mpangilio katika eneo hilo kugusana na kuzua hofu kubwa kwa wafanyazi wa jengo hilo na hasa wale waliokuwa ghorofa za juu ambao waliminyana katika ngazi ili kuwahi kujiokoa maisha yao kutokana na lifti zote kuwa zimezimwa kwa wakati huo na wengine kuogopa hata kurejea ndani ya jengo hilo hata baada ya kuzimwa kwa moto huo na wafanyakazi wenyewe kabla ya kufika kwa gari la zimamoto la Manispaa ya Ilala na kukuta shughuli hiyo imesha shereheshwa na wenyeji.

Wafanyakazi na wakazi wa jijini Dar es salaam, waliofika kupata huduma ndani ya jengo hilo wakiwa nje ya jengo hilo baada ya moto kuzimwa wakiogopa kuingia ndani.

Hizi ni nyaya za umeme zilizosababisha mtafaruku huo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.