Habari za Punde

*JK ZIARANI MKO WA KIGOMA, AZINDUA HOTELI MPYA TA LAKE TANGANYIKA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana, katika ziara yake mkoani humo iliyoanza leo. Kushoto ni Mmiliki wa hoteli hiyo, George Nzunda (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Simbakalia.Picha Zote na Frddy Maro


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mandhari ya Hoteli ya Lake Tanganyika muda mfupi baada ya kuifungua mjini Kigoma leo mchana. Kulia ni Mmiliki wa Hoteli hiyo, George Nzunda na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa kigoma Kanali Simbakalia.

Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, muda mfupi baada ya rais kuwasili mjini Kigoma leo mchana kwa ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Kanali Joseph Simbakalia.

Rais Jakaya akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli hiyo...

Baadhi ya wakazi wa kigoma wakimlaki Rais kikwete kwa ngoma za utamaduni baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma kwa zaiara ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.