Habari za Punde

*MILITARY FUN! KAZI YA JESHI SI MCHEZO JAMANI

Hii ilikuwa ni zoezi la kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia mbwa wa Polisi, ghafla mbwa alimgeukia askari na kuanza kumng'ata. Sasa sijui mbwa huyu alihisi kuwa na huyu jamaa ni miongoni mwa waandamanaji ama mbwa huyu hakuwa na mafunzo kamili kama wenzake?????

Ebwana eeh! kumbe hata jeshi pia ni usanii hebu angalia askari hawa ukuwa mbali, waweza hisi wote wana siraha kumbe wengine wanaigiza tu cheki katika mikono iliyozungushiwa alama nyekundu....

Afande japo anamsachi Mwanamama lakini pia naye anaogopa na hii sijui kama ni sahihi kwa mwanamam kusachiwa na mwanaume...au ndo vile kijeshi jeshi???


Hata uwapo lindoni njaa haina simile bwana unaweza kusahau hata silaa yako kama afande huyu hebu mcheki alivyojisahau na kuweka silaa kando huku akiendelea na zoezi la kusaka kitoweo.

Mmoja kaucha usingizi kiaina wakati wenzake wapo makini na tukio fulani kulia kwao wote kwa pamoja hata kumshtua mwenzao????? . Kesho nitawaleteeni matukio mengine ya hatari zaidi na ya kuchekesha ya jamaa hawa....usikose kupitia katika ukurasa huu wa sufianimafoto hapo kesho.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.