Habari za Punde

*NMB YAKABIDHI GAWIO KWA WANAHISA WAKE, WAANDISHI WATIMULIWA UKUMBINI

Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijo (kushoto) akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. milioni 721, 443, 385, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Sabetha Mwambenja, wakati wa hafla ya Benki ya NMB, kukabidhi malipo ya Gawio kwa wnahisa wake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wapili (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi NMB, Misheck Ngatunga na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ben Christaanse.

Mwenyekiti wa Bodi NMB, Misheck Ngatunga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ben Christaanse, wakimkabidhi mfano wa hundi kwa niaba ya serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijo, wakati wakati wa hafla ya Benki ya NMB, kukabidhi malipo ya Gawio kwa wnahisa wake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa benki ya Rabo akikabidhiwa hundi.

Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya Exim, Ms. Linda Chiza (kushoto) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa waliofika kupokea Gawio lao katika hafla hiyo.

Hawa ni baadhi ya waandishi wa habari walioondolewa kwenye Ukumbi wa mkutano wakati wa Hafla hiyo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa benki ya NMB, hapa wakiwa nje ya ukumbi huo wakisubiri kufanya Interview ili kujua kilichojili katika hafla hiyo. haikuweza kufahamika chanzo cha Shynaniliu kuwaondoa ndani ya ukumbi huo akidai hawaruhusiwi kuwamo na kusikiliza ukumbinu humo hali ya kuwa waandishi hao walialikwa na wahusika waliokuwa wakipokea Gawio hizo.

Ilibidi waandishi hao kuganda mahala hapo wakiwasubiri wapiga picha wao ambao nao pia waliingia ukumbini humo na baadhi yao wakaondolewa kwa kuvutwa mashati na Naniliu, akiwataka kuwa nje ya ukumbi huo huku mmoja akisikika akijitetea, mie nimeitwa na Exim lakini mwanamama huyo hakutaka kusikia lolote zaidi ya kumwambia. "Nimesema toka nje au unataka nikuitie askari wa hoteli"?

Hawa nao ni baadhi ya waandishi waliojionea karaa na kuamua kwenda kujisevia maakuli kuliko kuendelea kusemezana na mwanamama huyo.







No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.