Ebwana eeh! hawa wajenzi eti ni kwa nini huwa wanashindwa kujijali ama kujali maisha yao kwa ujumla, kama hawa jamaa walivyokutwa na kamera la Sufianimafoto, wakiendelea na ujenzi wa ghorofa lililopo pembeni ya ghorofa la PPF Tower, jijini Dar es Salaam leo mchana. Mara kadhaa kumekuwa na matukio ya wajenzi kuporomoka kutoka ghorofani wakati wakiwa katika shughuli za ujenzi, lakini inakuwaje mpaka sasa wakandarasi wanaowaajiri wajenzi hawa wanashindwa kuandaa vifaa vinavyowawezesha kufanya kazi kwa usalama zaidi, Hebu mcheki huyu jamaa amening'inia kama popo huko juu hata kamba basi ya kumnusuru ana kumuokoa pindi itakapotokea bahati mbaya ya kutaka kuanguka imuokoe hana, Je Wakandarasi mtawajali lini wafanyakazi wenu???
BIG UP KWA KAMPUNI ILIYOJITOLEA KUJENGA VIFAA HIVI VYA KUHIFADHI TAKA KATIKATI YA JIJINI
Iwapo yatajitokeza makampuni mbalimbali na kuamua kujenga vifaa kama hivi vya kuhifadhia taka katika maeneo ya jijini, basi angalau tatizo la utupaji taka hovyo linaweza kupungua kwani hata ungekuwa ni wewe unaweza kuwa ukijionea aibu kutupa hata kipisi cha sigara wakati unajua kuwa katika safari yako mbele waweza kukutana na kifaa kama hiki na kuhifadhi uchafu. hiki ni kifaa kilichojengwa karibu na jengo la Sukari House mitaa ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam, ambapo katika barabara hiyo vimejengwa vijidude kama hivi kadha. Wananchi wakiwezeshwa wanaweza japo utamaduni huo haupo tangu awali...

No comments:
Post a Comment