Habari za Punde

*TFF YAPATA HASARA MCHEZO WA KIRAFIKI WA BRAZIL NA TAIFA STARS








Na Sufianimafoto Reporter, jijini
Mchezo wa kirafiki wa Kimataifa baina timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Brazil, uliochezwa Juni 7 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imeelezwa kuwa mchezo huo umeingiza hasaba badala ya faida katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.
Akizungumza na wandishi wa habari Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kabumbu nchini, Frederick Mwakalebela, amesema kuwa mchezo huo uliingiza kiasi cha Sh. Bilioni 1. 7 tu.
Aidha alisema kuwa haijawahi kutokea kupata hasara na mapato kiduchu kama hayo katika michezo yote iliyowahi kuchezwa katika Uwanja huo.
Katika hatua nyingie katibu MWAKALEBELA amesema katika mchezo huo wa kiarafiki kati ya TANZANIA na BRAZIL wachezaji sita wa Taifa Stars, wameonekana na kupendwa na baadhi ya nchi kutokana na kiwango chao kizuri walichoonyesha siku ya mchezo huo, kutokana na mchezo huo kuonyeshwa katika nchi 160 duniani siku hiyo.
Hivyo TFF inamatumaini na wachezaji hao huenda wakapata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.