Habari za Punde

*SHUGHULI ZA RAIS JAKAYA KIKWETE WIKI HII

*WANAFUNZI WA VYUO VIKUU DODOMA WAANDAMANA KUMUUNGA MKONO JK, KUCHUKUA FOMU YA URAIS KATIKA UCHAGUZI UJAO.Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani Dodoma wakiwa katika maandamano ya kuumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete, ili kuchukua fomu ya kugombe nafasi ua Urais katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu. Maandamano hayo yalianzia katika Ofisi za CCM mkoa wa Dodoma leo mchana na kupokelewa katika Viwanja vya Nyerere Square.

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM, wakiwa na bango katika maandamano hayo.

*JK, AKUTANA NA MTEMI MPYA WA MASANZA MAGU
Rais, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mtemi mpya wa Masanza, Magu, Frederick Ntobi, al- maarufu kama 'Nyalubamba wa Pili' wakati Rais alipotembelea Kituo cha Utamaduni wa Wasukuma cha Bujora kilichopo Wilaya ya Magu. Kulia ni mke wa Mtemi, Joyce Bazira al-maarufu kam 'Ngole'.
*RAIS JAKAYA KIKWETE, AKUTANA NA WAKUU WA MIKOA, WILAYA NA MAKATIBU TAWALA.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na Waziri wa Tawala
za mikoa na Serikali za mitaa Selina Kombani wakiingia katika ukumbi wa Zamani wa bunge
kwaajili ya mkutano uliowajumuisha Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa wilaya uliofanyika mjini
Dodoma leo na kesho.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akizungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao cha pili cha Rais na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, kwenye ukumbi wa Msekwa Mjini Dodoma leo mchana. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wakuu wa Mikoa, wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete, katika kikao chake na Wakuu hao, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kwenye ukumbi wa Msekwa Mjini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe waloshiriki katika mkutano wa Wakuu wa mikoa na Wakuu wa wilaya mjini Dodoma na kuhutubiwa na Rais Jakaya Kikwete. Picha na Freddy Maro
Baadhi ya wajumbe waloshiriki mkutano wa Wakuu wa mikoa na Wakuu wa wilaya mjini Dodoma.
*JAKAYA AHUDHULIA MAZISHI YA MKE WA MDOGO WA MENGI MOSHI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Bi. Millie Benjamin
Mengi, wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika Machame, Mkoa wa Kilimanjaro jana mchana.
Marehemu Millie Benjamin Mengi ni mke wa Bwana Benjamin Mengi ambaye ni mdogo wa mwenyekiti wa makampuni ya IPP Bwana Reginald Mengi. Picha na Freddy Maro.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho kwa marehemu Millie Benjamin Mengi
Machame, mkoani Moshi jana mchana.































No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.