Na Jonathan Tito, Jijini Dar es Salaam
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, leo imeichapa timu ya taifa ya vijana ya Malawi kwa mabao 11-0 katika mchezo uliyochezwa leo asubuhi.
Katika mchezo huo uliyochezwa asubuhi Tanzania, waliutawala mchezo huo tangu dakika za mwanzao za mchezo, huku kikosi hicho kikiongozwa na washambuliaji wake hatari, Thomas Ulimwengu na Jarome Lambele.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika vijana wa Tanzania waliokuwa na uchu wa magoli, walikuwa kifua mbele kwa mabao 3, yaliyowekwa kimiani na Thomas Ulimwengu ambaye alipachika mabao mawili na Himid Mao alilofunga kwa njia ya penatli.
Tanzania waliingia kipindi cha pili kwa kasi ileile huku wakiendelea kulisakama lango la Malawi kiasi cha kuwafanya Wamalawi hao kuchaanganyikiwa.
Mabao yaliyopatikana kipindi cha pili yalifungwa na Ibrahim Rajabu, mabao mawili, Issa Rashid mabao mawili, Thomas Ulimwengu, Himid Mao kwa njia ya penalti na Jarome Lambele mabao mawili.
Pia katika mchezo wa jioni baina yao na Namibia, Vijana wameweza kuibuka washindi kwa mabao 2-1 mabao yaliyofungwa na Thomas Ulimwengu na Thabiti. Kila la Kheri timu yetu ya Vijana tuzidi kuwaombea ili wazidi kufanya vyema katika michezo iliyosalia.
KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA CMA KWA UANZISHWAJI WA MFUMO WA KIDIJITALI.
-
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Tume
ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa uanzishwaji wa Mfumo wa Uendeshaji na
Us...
3 hours ago
No comments:
Post a Comment